Bongo Star Search Waache Human Abuse, BASATA na TRCA wawaangalie !

True
 
Ndio maana nashangaa watu kama BASATA wanalea huu udhalilishaji.
 
Shindano ni kama lilikua na lengo zuri ila uendeshwaji wake ni mbovu sana hasa majaj....
Mtu anaingia kabla hajaonesha ujuzi wake wanamtoa confidence kwa vijembe au kumdhiaki, sasa mtu anashindwa hata kufanya kile alichojiandaa nacho.. Kumbuka anayekuja pale ni mtu anayetafuta namna ya kutoboa tu kwenye maisha na sio kwamba tayari yeye ni star...
Unakuta jaj anaacha ku comment juu ya uwezo wa kuimba anakua busy kudhiaki uvaaji wa mtu, kwan hapo studio hapakua na reception washiriki wakapewa angalizo?
Majaj wanakua na mambo ya ajab ajab sana hawajui ni kipi hasa cha ku jaj,na sometimes wanaonesha kabisa kumpendelea mshiriki fulan, mfano final iliyopita mtu anasimama na kumsimanga mshiriki kuwa hajui kuchagua wimbo na mtu alishafika final!!!yaan una mchongea njia mshiriki mwingine na huku ungeacha chance iwe 50/50 tu.

Hata hao majaj wenyewe wengine hata kuimba hawajui, ukienda you tube uko kuna clip madam ritta anaimba ma flat tu, out of tempo wapogaji wa vyombo wanamuokota kila mara lakin eti yeye ndio chief Judge ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Kweli BSS n mrad wao lakini wawatendee haki wa tz
 
Tuseme ukweli kuwa BSS bado haijaleta matunda kwa tasnia ya Muziki Tanzania, wasanii wao wanaotokaga katika mashindano hayo huishia kwa kuonekana tu msimu wa BSS baada ya hapo hupotelee juu mawinguni.
Vipi kuhusu American Idol , The Voice na America's Got Talent ina matunda gani huko nchini mwao,tuweke kumbukumbu vzr.
Naomba vielelezo viletwe mezani mheshimiwa.
 
Wale majaji wote umri umeenda hakuna mwenye ndoa inayoeleweka ndo maana wanawaletea vijana stress.

Kuna yule kijana Sasa hivi yuko kundi la mabantu na ameshatoka ,wakati hajatoka alienda bss salama akamwambia hujui kuimba rudi nyumbani kapike
 
Tuseme ukweli kuwa BSS bado haijaleta matunda kwa tasnia ya Muziki Tanzania, wasanii wao wanaotokaga katika mashindano hayo huishia kwa kuonekana tu msimu wa BSS baada ya hapo hupotelee juu mawinguni.
Huwezi kupata mastaa kupitia program hii sababu hakuna majaji maPros kwenye hiyo fani bali majaji ni watu wa deal..wangeweka majaji mapros halafu wao wakawa executive committee ya kutoa maamuzi lakini kwa kufuata ushauri wa kitaalam
 
Hili Mimi nililiona nikaliandikia kwakeli hawa majaji sio wastarabu kabisa!!!
They think wapo heaven!!!
Nimwendo. Wa udhalilishaji tu
 
Huyo Salama anatumia lugha mbaya na maneno ya ovyo mno! Ni kama hajakua, ni sawa na mtu ambaye hana exposure, anaropoka, anapanic halafu ana kaubabe flani ka kishambaaaaaa
Angekuwa na chura sijui ingekuwaje

Hapo flat screen tu jeuri anajiona star kamaliza

Ova
 
Hapa ndipo huwa nashindwa kuwaelewa wabongo kabisa. Hawajui njia za kutatua matatizo yao, wao ni kulalamika tu hata kwa mambo madogo. Wewe (na wote) wenye maoni kama yako njia nzuri kabisa ya kukomesha ujinga kama huu ni kutokungalia kipindi. Wakikosa watazamaji, kitakufa natural death. Na hao vijana kwa nini wajipeleke sehemu kama hiyo? Wanalazimishwa? Watanzania tuache kutegemea serikali zembe kama hii itufanyie kila kitu. NB: Unacholalamikia kinaweza kuwa ni kweli (mimi siangalii ujinga kama huu, hivyo sijui) lakini uwezo wa kuchukuwa hatua mnao watazamaji na hao washiriki.
 
Point sana umetema

Maana sisi wengine hiyo bss hatuiangalia miaka kibao sahvi

Wabongo wakati umefika wakiona vitu ndivyo

Sivyo waachane nayo tu

Ova
 
Wewe naye mimi hapa nalalamika au naongea kwa nilichokiona.
Square your mind kabla hujaandika kitu.
FYI mimi sio shabiki wa hiki kipindi.
 
Wewe naye mimi hapa nalalamika au naongea kwa nilichokiona.
Square your mind kabla hujaandika kitu.
FYI mimi sio shabiki wa hiki kipindi.
Umelalamika bila kujua kuwa umelalamika? BTW kama wewe siyo shabiki haya umejulia wapi? Ili mtu uweze kuandika hivyo ni lazima uwe unaangalia mara kwa mara.
 
Umelalamika bila kujua kuwa umelalamika? BTW kama wewe siyo shabiki haya umejulia wapi? Ili mtu uweze kuandika hivyo ni lazima uwe unaangalia mara kwa mara.
Kwa hiyo unanijua kuliko navyojijua???
We kiazi kweli, acha nikupuuze.
 
Kwa hiyo unanijua kuliko navyojijua???
We kiazi kweli, acha nikupuuze.
Kwani ni ajabu mtu kutokujitambua? I mean, hujui unaweza kuwa hujui lakini hujui kwamba hujui? Ni wengi wadhani wao ni werevu kumbe sivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ