Kweli kabisa, umenikumbusha kuna ka mamz kangu kamoja baada ya kuona koki ya hela nimemfungia akapata boya mwengine ambaye anatuma hela kila anapopigwa mzinga. Dharau zikawa nyingi sikujua kumbe ndio kashapata huyo fala. Huyo jamaa anafanya business ya madini ana hela ila mshamba wa chupi.
Kuja kusanuka nikamchukua maelezo mtoto ni kuwa huyo jamaa alikuwaga anamtaka long time toka enzi yuko mmbichi ila hakuwahi mpenda ila sahivi kamfungulia njia kwa sababu hali ya life ni tete na yeye anakiri anapenda hela sana. Kashachoka anataka aolewe zake na mwanaume wa kumhudumia kila akiwa na shida nikamwambia no sweat, mi kwakuwa na akili timamu siwezi kwama, najua ntapiga K nikitaka ila majukumu mengine atasimamia huyo Boya. Kwangu ikawa nafuu maana nshatoboka sana ila ule mziki nikagundua ni CD700 sitauweza.
Sasa demu anawaza kuja kuwa mwanamke flani hivi kama icon kwa mbeleko maana anapenda maisha ya juu hela hana. Mbaya zaidi akili ya mawazo ya kujenga pia hana. Yuko much on dependance yeye alie shida apewege tu hela ajaze vitu ndani kwake na kuvaa sana bila kusahau kodi ikiisha alipiwe.
Sasa imagine jamaa akioa huyu demu kitakachotokea ni kwamba demu anaweza akapewa life kiuhakika maisha ya kuendesha Rav 4 au Xtrail sio haba. Mbwembwe atakazokuwa nazo ila ukichunguza deep down ni msela kamenyeka ila watu watamuona super woman.🤣🤣🤣🤣🤣