Bongo uaminifu na kuaminiana waislamu wako mbali sana

Bongo uaminifu na kuaminiana waislamu wako mbali sana

Ilo kwa muislam mwenye dini kwenye pesa ondoa shaka ila nikutahadhirishe usije ukaamini same kwenye kumwachia mkeo huko wengi hua wadhaifu sana ila kwenye pesa dhurma hua tunaogopa kupita maelezo.
Kwamba mashehe wanapenda Sana Chini[emoji4]
 
Sahii kabisa
Wale waislamu jina Wala kitimoto na bia hawapaswi kua kundi hili.

Nnaoqazungumzia ni wale washika dini haswa na swala 5 na wacha Mungu[emoji4]
Washika dini sana wanayale madubwasha yao ambayo husema hayana shida
 
Waislamu washika dini hasa na ambao wako kwenye biashara kitambo ndio hao wengi wana uaminifu mkubwa sana...otherwise wengine waliosalia utajuta ukiingia anga zao na ndio wapigaji wengi hapa mjini...kigezo cha dini kisikufanye ukamwamini mtu kwenye biashara
 
Siyo kila mwislam mwaminifu wewe, wapo kina Rashid wengi matapeli hapa mjini, limoja linaitwa Hassan kudadeki zake.
Kenge kati ya mamba...hata huku kwetu ambako tunatuhumiwa upigaji sio kwamba ni wote
 
Waislamu washika dini hasa na ambao wako kwenye biashara kitambo ndio hao wengi wana uaminifu mkubwa sana...otherwise wengine waliosalia utajuta ukiingia anga zao na ndio wapigaji wengi hapa mjini...kigezo cha dini kisikufanye ukamwamini mtu kwenye biashara
Wafanyabiashara karibu wote wapo kwenye kundi hili
wizi
au
Ushirikina
Watakataa sana ilaa hilo kwa kilamtu kwa wakati wake atajithibitishia au ndan ya moyo wake anajua ukweli ila atapinga tu.
 
Nasubiri waje na hoja sio pinga pinga tu
Waje? Umejifunua. Hauna ukristu wala ukatoliki wowote. Kuweza kuwakumbuka, ni dhahiri kuwa ni exceptional. Wapigaji wako katika dini zote sio yenu tu. Kama vile vibaka wako wakina Mudi na wakina Joni. Kitu muhimu ni wewe kuwa muaminifu na kumpima mtu kwa anavyokutendea na sio kwa dini yake.
Acheni kuingiza udini katika kila kitu.

Amandla...
 
Binafsi Ni mkristo mkatoliki na Niko kwny biashara Zaid ya miaka 18 sasa

Ila kiukweli jamii ya waislamu hasa wa Zanzibar, somali au bara wale wazee wa swala 5 Ni waaminifu sijapata kuona.

1. Kuna msomali mmoja mwaka 2008 ile bado mchanga biashara, hanijui simjui ndo mara ya kwanza nanunua mzigo kwake, ila aliniamini akanikopesha mzigo wa pesa ndefu kwamba nikishauza ntamtumia pesa zake. Kweli nikamrejeshea kwa uaminifu na tunafanya biashara vizur Hadi leo. Hatujawai dhurumiana hata Senti.

2. Kuna mpemba mmoja ni nafanya nae biashara yuko nje ya nchi mwaka wa 4 huu, simjui hanijui, Zaid ya calls na chats kupitia wasap, nilitumiwa TU namba kupitia mtu baki, ila uwa namtumia pesa ananitumia mzigo na mizigo mingine ananikopesha. Tunafanya biashara Safi kwa upendo wa Hali ya juu utadhani mtu na ndugu Yake.

3. Kuna ustadh mmoja msambaa anamiliki mpesa matawi kibao Hapa k'koo mengine kibaha na mbezi . Ila matawi yote mengine yanayosoma till za jina lake, kaweka mashehe wenzie waliokutana na kufahamiana mskitini na wanayamiliki na kuendesha 100% ili kutunza familia zao. Ustadh yeye kabaki na matawi 2 tu anayoyamiliki 100%.

4. Kuna mfanyabiashara mwenzangu Ni mrangi wa dodoma ila Ni shehe swala 5. Yeye tangu nimjue hajawahi kukopa pesa ya riba benki yoyote Hapa nchini, kwake riba Ni haramu.
Akiwa na shida na pesa au mtaji umeyumba anaazima kwa mashehe wenzie uko mskitini na kurejesha Kama zilivyo.

5. Kuna mwislam mmoja mrangi Yuko Moro, nmemtumia sana kipind flan nafanya biashara ya nafaka. Huyu Tumejuana TU barabarani Tena kijiwe Cha draft, nikawa namtumia pesa ananikusanyia nafaka na kupakia kwny fuso na kunitumia dar. Ila mpaka naacha ile biashara, hajawahi nidhurumu hata Senti moja. Tuna maelewano mazur Hadi Leo.

6. Mwingine Ni shehe mmoja msomali agent binafs wa magari used yuko japan, ila ana wateja wengi Tanzania ,Zambia Hadi Uganda na Congo. Mteja analipia,gari inasafirishwa Hadi Uganda,Zambia kwa uaminifu mkubwa.
Anasifiwa Sana uaminifu kule kwny uzi wa magari used japan.

7. Mwingine Ni mpemba mmoja shehe anajiita Abdulwahid Yuko zanzibar anauza tv Toka Dubai, anasifiwa Sana kwa uaminifu kule Uzi wa wauza tv. Nami pia nishafanya nae biashara,hanijui simjui, Nikamtumia pesa ndefu akanitumia mzigo wangu Safi kabisa nikaupata Bila longolongo.

Mifano Ni mingi Sana,
Ila nikiri waislamu wako mbali Sana kwenye suala zima la uaminifu.

Nawasilisha[emoji1431]
Uaminifu Vs Hofu
Hivi vitu husababishwa na nini?
 
Bado hujakutana na majambazi , matapeli na washirikina.

Kwa umri huu usitake kunidanganya mkuu, binadamu ni watu hatari kuliko hata maelezo.

Naheshimu tu dini na taasisi za watu ila kuna watu wachafu na wanajificha kwenye dini ila hawajakupatia tu pazuri wakupige.

Wanapigana huko huko na wanamalizana kimaya kimya.
 
Sahii kabisa
Wakristo wengi uaminifu Changamoto Sana, binafs nikifanya dili na shehe yoyote nakua na amani Sana[emoji4]
.
JamiiForums-454900825.jpg
 
Back
Top Bottom