Bongo Vifurushi vya Simu Bei Bwerere!!!

Bongo Vifurushi vya Simu Bei Bwerere!!!

Mara kadhaa utawasikia wabongo wanalalama saaana, kwamba kampuni fulani ya simu, vifurushi vyake ni ghali sana, na hivyo watahamia kwa mpinzani.

Bila shaka wengi wao hawajui kwamba vifurushi vyetu ni bei chee sana. Kuna nchi za Afrika ambazo kupiga simu na kutumia mobile data ni anasa kubwa.

Afrika kusini, ukiwa na MTN huwezi pata 1GB ya wiki 2 kama huna zaidi ya Tsh 25,000/=.

Jirani Kenya, SafariCom wanauza 1GB ya mwezi kama kwa Tsh 10,000/=.

Rwanda 1GB ya wiki MTN wanafanya zaidi ya Tsh 15,000/=.

Wakati Uganda 1GB ya week inauzwa na MTN kwa Tsh 8,000/=.

Hebu linganisha hizo gharama na upatacho Voda, Tigo, Airtel, Halotel na Smart!!!
Ebu na wewe kama umekopi sehemu changanya na za kwako. Je, Tsh 10,000 kwa hela ya Kenya ni sh ngapi? Na Je, wanatumia mtandao mmoja tu wa MTN? Je, unaweza kuhitimisha kwa mfano Tanzania mtandao mpya wa Halotel na kusema Tz mitandao ni cheap??????. Think Big. Kwa mfano, Tsh 25,000 ni sawa na ngapi kwa Afrika ya Kusini??????
 
Tusilalamikie viongozi wetu, kwasababu uchumi wa Tanzania unakua kwa 6%+ wakati ule wa marekani kwa chini ya 2%
 
Mleta uzi huu utakuwa unatumiwa na makampuni ya simu ili mhalalishe Wizi wenu wa data package, huwezi kulinganisha bei ya package za data au airtime pasipo kulinganisha na economic capability ya nchi hizo na yetu. Huu wizi wa makampuni ya simu kupitia data package TCRA waudhibiti. Na wewe mleta uzi huu waambie tumekataa Wizi huu[emoji16][emoji16]
 
Natumia MTN 2GB kwa wiki ni R99 sijui ni kiasi gani kwa bongo ila haizidi Tshs25000 na 1GB ni R89 kwa wiki 2 wacha kudanganya watu blaza.
 
Bora bei yake ingekuwa juu ila ukataji wa hizo GB/MB ukawa mzuri. Si kwa makato haya aisee, GB 1 inaishia kwa muda mfupi sana.
Duhhhhh,kwahiyo tunauziwa GB/MB hewa,
kila kitu ni hewa
 
  • Thanks
Reactions: t2t
Alichokosea mtoa mada ni kutoa absolute comparison.. Anapaswa kutoa relative comparison amabyo ina consider contextual factors. Unaposema kitu fulani ni ghali au rahisi lazima iwe relative to something labda cost of living au kipato
 
Unakosea kulinganisha hizo bei bila kuangalia pia pato la watu...kwa mfano pato la mmoja mmoja kwa mwezi katika nchi ulizotaja alifanani kabisa hivyo hata level ya manunuzi inaweza kuwa tofauti kabisa....

Naamini kabisa mfanyakazi wa serikali wa Tz anayelipwa mshahara wa laki 5 hawezi kununua kwa kifurushi cha data huko south na akafurahi...hii kwake inaweza kuwa ni mzigo mkubwa kulingana na pato lake
Umeongea kitu cha msingi sana ambacho huyu mleta mada(no doubt ni fisiemu) ana kikosa katika uelewa wake.

Gharama za maisha always ziko determined na overall income earning ya watu wa eneo husika na huwa hazifanani na maeneo mengine hata siku moja.

Leo ukimchukua mfanyakazi wa benki wa hapa bongo mwenye mshaara wa 700,000/= ukimpeleka south africa hata kuwa ni mmoja wapo ya watu wanaoishi maisha ya kimaskini sana na hawezi kuafford hzo gharama za simu comfortably kama ilivyo kwa hapa bongo.

Wakati huo ukichumkua mwalimu wa elementary school kutoka huko south africa anaelipwa rand 34,000 kwa mwezi ukamleta hapa bongo anaishi kama mkurugenzi wa TRA na maisha kwake yatakuwa ni marahisi sanaa.

Anachokosea na hasichojua huyu mleta mada ni kugeneralize as if wote tunatumia pesa moja,tunaishi mazingira sawa na changamotomo tulionazo ni sawa.

Ni ukweli usiojificha huduma za kijamii hapa bongo ni ghari sanaa kulinganisha na maeneo mengine mengi tu.
 
Ebu na wewe kama umekopi sehemu changanya na za kwako. Je, Tsh 10,000 kwa hela ya Kenya ni sh ngapi? Na Je, wanatumia mtandao mmoja tu wa MTN? Je, unaweza kuhitimisha kwa mfano Tanzania mtandao mpya wa Halotel na kusema Tz mitandao ni cheap??????. Think Big. Kwa mfano, Tsh 25,000 ni sawa na ngapi kwa Afrika ya Kusini??????

Kwanza kutuma pesa kutoka kenya kuja bongo gharama ni nafuu sana kuliko kutuma pesa kutoka bongo kwenda kenya kwa mobile transaction.. hii ni evidence tu kuonesha hayo maelezo yake hayana validity yoyote.

Hiyo Tsh.25,000 ni sawa na 140 rand, pesa ambayo inatosha kununulia ndala za kuogea tu huko afrika ya kusini.
 
Kwa mfano uliotoa wa ndala maana yake ingekuwa 2000tsh kwa tanzania
 
Back
Top Bottom