Bongo Vifurushi vya Simu Bei Bwerere!!!

Bongo Vifurushi vya Simu Bei Bwerere!!!

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Mara kadhaa utawasikia wabongo wanalalama saaana, kwamba kampuni fulani ya simu, vifurushi vyake ni ghali sana, na hivyo watahamia kwa mpinzani.

Bila shaka wengi wao hawajui kwamba vifurushi vyetu ni bei chee sana. Kuna nchi za Afrika ambazo kupiga simu na kutumia mobile data ni anasa kubwa.

Afrika kusini, ukiwa na MTN huwezi pata 1GB ya wiki 2 kama huna zaidi ya Tsh 25,000/=.

Jirani Kenya, SafariCom wanauza 1GB ya mwezi kama kwa Tsh 10,000/=.

Rwanda 1GB ya wiki MTN wanafanya zaidi ya Tsh 15,000/=.

Wakati Uganda 1GB ya week inauzwa na MTN kwa Tsh 8,000/=.

Hebu linganisha hizo gharama na upatacho Voda, Tigo, Airtel, Halotel na Smart!!!
 
Hata Bongo ukigusa vifurushi vya Wiki au Mwezi bei ni zaidi ya Hizo, usitetee kitu usichokijua
 
Badala ya huu usanii wa vifurushi kwanini Huduma zisiwe reasonable tukawaelewa?
 
Tunaomba 'source' yako, vinginevyo wewe ni mmoja wao tu!

TTCL mko wapi? Hebu tuondoleeni hawa wezi wa 'data packages', TUMECHOKA!
 
Voda sahv 24 hours mb elfu 2 ! Unataka waongeze ?
 
We utakuwa na maslahi hv tz utafananisha na south africa
 
Kuna kipindi tigo ilikuwa unapiga simu bure daily ukilipa 1500 tuu,

Ila naona muziki wa data unawaelemea sana sio tigo tuu mitandao yote nimetumia tigo, airtel, zantel, voda, smart, Halotel, sasatel, kote huko vifurushi vya data ni ngumu kumesa,
Kwa sasa tatu bora kwenye data ni

1. VodaCom Tz
2. Halotel Tz
3. Airtel Tz
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Watu wengi wanasema ni rahisi kwa sababu wanakimbilia katika vyuo vikuu kwenda kujiunga. Kumbuka hata aya makampuni ya simu yalikuwa yanapeleka kodi ndogo sana serikalini, sasa ivi yatapandisha viwango
 
Unakosea kulinganisha hizo bei bila kuangalia pia pato la watu...kwa mfano pato la mmoja mmoja kwa mwezi katika nchi ulizotaja alifanani kabisa hivyo hata level ya manunuzi inaweza kuwa tofauti kabisa....

Naamini kabisa mfanyakazi wa serikali wa Tz anayelipwa mshahara wa laki 5 hawezi kununua kwa kifurushi cha data huko south na akafurahi...hii kwake inaweza kuwa ni mzigo mkubwa kulingana na pato lake
 
Watanzania uzuzu na uelewa kufikiria mbali hatuna, utakuta mtu kashupaa anabisha sababu ya ulayman wake anajifanya kuongea ongea bila vigezo..!
 
Kuna kipindi tigo ilikuwa unapiga simu bure daily ukilipa 1500 tuu,

Ila naona muziki wa data unawaelemea sana sio tigo tuu mitandao yote nimetumia tigo, airtel, zantel, voda, smart, Halotel, sasatel, kote huko vifurushi vya data ni ngumu kumesa,
Kwa sasa tatu bora kwenye data ni

1. VodaCom Tz
2. Halotel Tz
3. Airtel Tz
Halotel kwa data wako vizur usitudanganye
 
Back
Top Bottom