Bongofleva: 5 Biggest Losers and Winners

Bongofleva: 5 Biggest Losers and Winners

mziki wa bongo fleva bila sugu kweli????

alikiba au Ay wana mchango na muziki kuliko sugu???

au wamefanikiwa kuliko sugu??

hata lady jaydee ametolewa na sugu.. mara ya kwanza kwake kuimba ni chorous ya mambo ya fedha nyimbo ya sugu enzi hizo..

na sugu ndio kamwambia prof jay njoo chadema twende bungeni tunaendeleze harakati..
 
Mkuu list yako imekaa vyema.Kidogo naona tu AY umempa upendeleo mkubwa.Ni kwel anastahil lakin sio kuwa nafas ya pili.
Ommy dimpoz anajikongoja sio mbaya angekula mentio.Navy kenzo bado ni asubuh sana kuwapa crdt.
Otherwise kaz nzuri mkuu
 
Matonya alitakiwa awepo qchief walisumbua Sana na Sam wa ukweli sijui kapotelea wapi
 
Hata mi nilitaka nishamgae dudubaya alianza kusumbua Sana na hiyo mwanangu huna nidhamu miaka 2007 akarudi na nyimbo amevaa manguo meusi ya kitamaduni halafu baada ya hapo akapotea yaani.
Mimi nimeisikia hiyo ngoma 2001 au umechanganya madesa mkuu
 
mkuu umejitahid ila bado Mr Blue angepaswa kuwepo. ivi ule upande wa dansi huangalii huko?
fid q,
 
Mimi nimeisikia hiyo ngoma 2001 au umechanganya madesa mkuu
hapana wewe ndo hukunielewa labda sababu sijaweka alama ya mkato nimemaanisha miaka ya 2007 akarudi na nyimbo nyingine hivi jina nimelisahau haalafu akapotea.
 
Huwa najiukiza sana inakuwaje msanii akiyeandika nyimbo moja ya nyimbo kali kwenye historia ya Bongofleva anapoteza direction mpaka anakunywa komoni??? Dah sijui alikosea wapi jamaa
walimwengu wanakatisha sana tamaa. majungu/maneno yanakwaza sana mtubunaumia ati
 
mkuu umejitahid ila bado Mr Blue angepaswa kuwepo. ivi ule upande wa dansi huangalii huko?
fid q,
Mr Blue angekaa wapi mkuu? Kwenye losers au winners? Maana kote hapo naona hafiti, hatuwezi kusema ni looser kwasababu bado anafanya mziki na anafanya poa kiasi chake lakini pia hatuwezi kusema ni winner kwasababu ameshuka sana hayupo kwenye ubora wake kama kipindi kile alipoitikisa Bongofleva!!
 
Nature vepe!
Dah! Nimepata wakati mgumu akae kwenye list ipi? Maana kimuziki ameshuka so hawezi kuwa kwenye list ya winners but pia huwezi kumuweka kwenye list ya losers coz kitaa bado watu wanamkubali sana, we andaa shoo alafu muite, anakujazia ukumbi nyomi ya kufa mtu
 
Mtoe Kiba, aingie Mr 2 Sugu..

Na huko kwenye losers mtoe Juma Nature aingie Marlaw..

Otherwise HESHIMA YAKO UMETISHA...!!
Daaah ila Nature sijui ananini tu mpaka leo hii akipanda jukwaani na vinyimbo vyake vya zamani mashabiki wanachanganyikiwa
 
Daaah ila Nature sijui ananini tu mpaka leo hii akipanda jukwaani na vinyimbo vyake vya zamani mashabiki wanachanganyikiwa
Jamaa ana 'nyota' kali sana ila basi tu, sijui ndio zama zake zimepita??
 
Hiyo list ya looser nafasi ya dudu baya alitakiwa akae Mb-dogy, dudu hajawahi sumbua zaid ya kuotea ile ngoma ya nakupenda. Maoni tu
na ninahisi alichangia kummaliza Mr Nice kiutamaduni... nimeoteshwa🙄
 
Mkuu, nilifikiria sana watu kama akina Sugu, Afande Sele au hata Solo thang lakini nikaja kugundua kuwa kumuweka mtu kama Sugu katika list ya 'loosers' haita kuwa na maana kwasababu ingawa kimuziki hayuko juu kama enzi zake lakini ameutumia umaarufu aliojijengea kwenye mziki kuanzisha harakati zake za kuitumikia jamii (siasa)! So Sugu ni mfano wa kuigwa, haitaleta maana akiwekwa kwenye list ya 'losers'..

Kwa kuongezea tu winners and loosers uliwaelezea ni 5/5 hivyo ni ngumu kum squeeze mahala, ila naamini kuna winners na loosers wengi sana bongo si hawa tu. Asante kwa hii thread
 
Kwa kuongezea tu winners and loosers uliwaelezea ni 5/5 hivyo ni ngumu kum squeeze mahala, ila naamini kuna winners na loosers wengi sana bongo si hawa tu. Asante kwa hii thread
Yeah, the list is long ndio maana nimeona niweke wachache tu ambao wameleta impact kubwa zaidi either kwa ku-lose au kuwin..
 
Back
Top Bottom