Boni Mwaitege ashusha mjengo wa hatari Kitunda

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,305
Habari wababodi,

Wengi walikua wanaulizia habari za Boni Mwaitege sana maana hajasikika mda mrefu kwenye medani za gospel.Msanii Mwaitege amefunguka kwamba yupo busy na biashara zake za kuuza maji na kulima.

Boni Mwaitege amefungua kituo cha kuuza maji maeneo ya nyumbani kwake Kitunda,Kinyantila,biashara inayomuingizia pesa mbali na kuuza maji pia analima mazao ya chakula.

Picha za chini ni mjengo wa Boni Mwaitege uliopo DSM,Kitunda Kinyantila na mabanda ya uani kwa ajili ya wapangaji.
Bonny Mwaitege House.jpg
Bonny Mwaitege2 House.jpg
 
Hongera zake kwa kuchagua kilimo.
 
Hiyo nyumba ya kawaida sana mbona mkuu,..nyingi ya aina hizo utazikuta maeneo vijijini...hakuna haja ya kuleta habari za kusema mjengo_ungeeandika nyumba tu.

Anyway_hongera sana Mwaitege umejikomboa na kodi.
 
Kwako ni ya kawaida ila kwa mleta uzi na sie wenzake wa singo na dabo za uswazi huo ni mjengo.
 
Maisha ni nyumba. Hongera zake kwa kusoma game vizuri. Kule kny entertainment jina kubwa, hela hamna, maisha duni. Mwishowe vijana wanakucheka eti umefulia.
 
Hiyo nyumba ya kawaida sana mbona mkuu,..nyingi ya aina hizo utazikuta maeneo vijijini...hakuna haja ya kuleta habari za kusema mjengo_ungeeandika nyumba tu.

Anyway_hongera sana Mwaitege umejikomboa na kodi.

Hongera kama kwako ni ya kawaida.
 
Kwako ni ya kawaida ila kwa mleta uzi na sie wenzake wa singo na dabo za uswazi huo ni mjengo.

Kwa maana nyingine hiyo nyumba haiendani na hadhi au umaarufu aliokuwa nao
 
Hiyo nyumba ya kawaida sana mbona mkuu,..nyingi ya aina hizo utazikuta maeneo vijijini...hakuna haja ya kuleta habari za kusema mjengo_ungeeandika nyumba tu.

Anyway_hongera sana Mwaitege umejikomboa na kodi.

Kula tano mkuu.
Eti mjengo.Khaa!
Hongera zake anyway maana bora hapo ataishi kwa amani kuliko kupangisha.
 
Wewe hata haujanielewa nimemanisha nini-hata haja ya kukuelewesha sina maake unateswa na unyonge na umasikini wa mawazo.....kwa heri mkuu

Ok, see u.....
 
Jambo jema kabisa hilo la kuwa na lijengo kama hilo.
 
Kula tano mkuu.
Eti mjengo.Khaa!
Hongera zake anyway maana bora hapo ataishi kwa amani kuliko kupangisha.

Nashangaa wengi humu hawana hata kiwanja lakini mabingwa wa kubeza wenzao. Kwani nyumba hata ya vyumba viwili huwezi kuita mjengo?
Acheni kutuzengua! Hongera Mwaitege!
 
Mada za kijinga kabisa!Ina maana hili ndio boonge la jumba!
 
Back
Top Bottom