Boniphace Jacob (Boni Yai)
ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pwani lakini pia amewahi kuwa Meya wa Kinondoni. Aidha kutokana na ajenda ya chama chake ya 'No reforms, no election' Boni Yai amekuwa mstari wa mbele katika kuisemea ajenda hiyo ili kuchochea mageuzi katika mifumo ya uchaguzi, hasa sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru, haki na uwazi.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakisambaza video iliyowekewa kichwa cha habari, "Boni Yai na Kanda ya Pwani waisaliti 'No reforms, no election' waiomba serikali warudi kwenye uchaguzi" huku katika video hiyo anaonekana Boni Yai akisema wapo tayari kwa ajili ya uchaguzi.
Je, uhalisia ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search pamoja na marejeo ya video imebainika matumizi ya video hiyo yanapotosha uhalisia kwani kauli hiyo Boniface Jacob
aliitoa Novemba 07, 2024 kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Boface Jacob alisema Mwenyekiti wa alisema wako tayari kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa namna na hali yoyote ile.
Aliyasema hayo siku ya Alhamisi Novemba 7, 2024 wakati akizungumza na wagombea wa Dar es Salaam wa nafasi za uongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 27, 2024.
“Kwa hatua tuliofikia hatutakubali ujiondoe wakati huu, kwa sababu yoyote…ukijiondoa kwenye mchakato kisha kukimbilia sehemu fulani basi utatukuta huko huko, ukijiondoa Kinondoni na kukimbilia Bunju utatukuta hukohuko, tutakurudisha kwa gharama yoyote,”