Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Pwani Boniface Jacob(Boni Yai) amekanusha kauli zilizokuwa zikisemwa na baadhi ya watu wanaojivua uanachama wa chama hicho akiwemo John Mrema kuwa ajenda ya 'no reform no election' sio halali na haikua na nia ya kuzuia uchaguzi bali ilikuwa inalenga kuteka umma(kupata attention).
Boniface ameeleza kuwa ajenda hiyo ni halali na niajenda ambayo imepitishwa na vikao halali vya kamati kuu ya CHADEMA.