Pre GE2025 Boni Yai: Mbowe utabakia kuwa Jenerali na kiongozi wangu siku zote, Nitakuwa tayari siku yoyote kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Leo sura imekushuka shuu..
 
Hakuna mshindi....chama kimeshashinda. Tumeshasema hongera kwa uongozi mpya. Kampeni zimeisha vijembe vimeisha sasa hivi ni ujenzi wa chama, October si mbali mambo ni mengi muda mchache.
Yerico na Ntobi warudi kujenga chama
 
Yerico na Ntobi warudi kujenga chama
Hilo ndilo la msingi kwa sasa na wao wameshakubali kwamba kampeni zimeshaisha makovu na visasi viponywe watu wasonge mbele kuivurumusha CCM madarakani.
 
Aulete ushauri kwenye vikao vya CC, twende na Lissu ndiye jemedari wetu sasa kamanda wa ardhini, majini na angani
 
Kwa maneno mengine Boni anaweka wazi ataendelea kuwa mtiifu kwa Mbowe, huu ni ujumbe mzito sana kwa Mwenyekiti mpya Lissu.

Lakini Boni, uliwahi kutuambia na tunaamini kwamba Mbowe anakusikiliza sana, ungempa ushauri mapema wa kujitoa kugombea wewe na yeye mngeyaepuka maumivu haya uliyotuandikia.

Hili ni andiko lenye maumivu makubwa na lawama kwa usaliti juu ya Mbowe. Boni na Mbowe mmesahau siasa ni mahesabu ya muda pia, ambapo nyie mlifeli.
 
Hii ya Boniyai ndio definition halisi ya "uchawa", sasa hivi mwenyekiti wetu mpya ni Tundu Antipas Lissu, tunatakiwa kumtii Tundu Lissu hata Mbowe anatakiwa kumtii Mwenyekiti Tundu Lissu, lakini pia tutaendelea kumuheshimu Mwamba Freeman Mbowe jabali la Siasa za Upinzani Tanzania.
 
Kura huamua mashindano,upande ulioshinda mnaungana nao mbona ni kawaida tu popote
sio rahisi kama unavyofikiria. Ndio maana viongozi wakichukua madaraka wanapanga safu ya watu wanaowaamini,, usidhani sugu, wenje, boni watamtumikia lisu kwa moyo mmoja, watamtumikia kiunafiki tu lakini rohoni wanataka afeli
 
Maana halisi ya CHAWA PROMAX
 
Kambi zote zilizozaliwa wakati wa uchaguzi wa CHADEMA zivunjwe mara moja.

Ndugu WanaCHADEMA muogopeni kama ukoma yeyote anayehubiri mgawanyiko ndani ya Chama.

STRONGER TOGETHER
 
Akubali kuendana na mabadiliko!
Bila hivyo hatakuwa na amani.
 
Ni kweli Kwa kuongezea ni kuwa Mbowe huwa sio mbinafsi wa kumfungulia mtu dunia.

Ukiachana na siasa kina Yericko , Boni na wengineo kuna faida kubwa waliipata baada ya kuwa karibu na Mbowe .



Ikiwemo fursa za kibiashara ,network n.k.

"Walipambania mtu na sio chama"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…