Pre GE2025 Boni Yai: Mbowe utabakia kuwa Jenerali na kiongozi wangu siku zote, Nitakuwa tayari siku yoyote kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maneno ya busara sana, uchaguzi umeisha na ni muda muafaka sasa kuruhusu CDM kufungua ukrasa mpya.
Tunautakia mafanikio mema uongozi mpya chini ya Antipas Tundu Lissu, tuna imani utawaunganisha wana CDM wote kuungamisha nguvu zao ili kwa pamoja sasa kulipambania Taifa letu.
Sherehe zimeisha sasa ni muda wa mapambano.

PIa tunamtakia Mh. Mbowe mapumziko mema, kama uongozi mpya ukimuhitaji kwa ushauri basi asisite kama alivyosema.kwa press yake ya hitimisho.

Best wishes.
Leo sura imekushuka shuu..
 
Hakuna mshindi....chama kimeshashinda. Tumeshasema hongera kwa uongozi mpya. Kampeni zimeisha vijembe vimeisha sasa hivi ni ujenzi wa chama, October si mbali mambo ni mengi muda mchache.
Yerico na Ntobi warudi kujenga chama
 
Yerico na Ntobi warudi kujenga chama
Hilo ndilo la msingi kwa sasa na wao wameshakubali kwamba kampeni zimeshaisha makovu na visasi viponywe watu wasonge mbele kuivurumusha CCM madarakani.
 
Maneno ya busara sana, uchaguzi umeisha na ni muda muafaka sasa kuruhusu CDM kufungua ukrasa mpya.
Tunautakia mafanikio mema uongozi mpya chini ya Antipas Tundu Lissu, tuna imani utawaunganisha wana CDM wote kuungamisha nguvu zao ili kwa pamoja sasa kulipambania Taifa letu.
Sherehe zimeisha sasa ni muda wa mapambano.

PIa tunamtakia Mh. Mbowe mapumziko mema, kama uongozi mpya ukimuhitaji kwa ushauri basi asisite kama alivyosema.kwa press yake ya hitimisho.

Best wishes.
Aulete ushauri kwenye vikao vya CC, twende na Lissu ndiye jemedari wetu sasa kamanda wa ardhini, majini na angani
 
Wakuu ujumbe wa Boni kwa boss wake wa zamani
==

Freeman Aikaeli

Mbowe Kwangu umekuwa siyo tu kiongozi wangu wa chama bali ni mwalimu, mwanafalsafa,mkufunzi,mzazi,mlezi na rafiki wa kweli. Wewe ni mfano wa kuigwaNashukuru kwa kuniamini na kunipa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kampeni zako katika uchaguzi mkuu wa chama January 2025.

Unajua,umeona, umesikia na umeshuhudia hadi sekunde ya mwisho nilivyo simama na wewe na nilivyojitoa kwa hali na mali kufanya jukumu lile zito lililokuwa mbele yetu lakini bahati haikuwa upande wetu.

Sikuwahi kufikiri au kudhani ipo siku mwalimu wangu wa siasa atanipa mimi mwanafunzi wake kazi ya kusimamia kazi yake ya siasa Hata hivyo nachezwa na machale, ninavyokufahamu itakuwa ulikuwa kuna kitu ulitaka nijifunze kwenye majukumu yangu ya kusimamia kampeni zako.

Moja ya funzo kubwa na la ajabu nitalikumbuka daima katika uchaguzi huu ni pale uliponieleza "Watu wako rasmi uliowapa jukumu la kufanya kampeni wasifanye Jambo lolote bila idhini yako, na pia katika kila jambo tutakalofanya tusikiumize chama kwa namna yoyote ile au kwa kisingizio chochote kile"Mapenzi yako kwa CHADEMA na wanachama wa CHADEMA ndiyo yalinifanya nikubali kubeba Jukumu hili zito,ulistahili "support" yangu hata kama Dunia nzima ingekusaliti kisiasa na kukugeuka bado mimi ningebakia peke yangu kuwa pembeni yako.

Ndiyo maana nilipoona kura zetu hazijatosha sikuhitaji ruhusa yako kusaini fomu ya matokeo kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu ni mshindiNa nilipokujulisha matokeo ya uchaguzi kuwa wajumbe 482 walihitaji uwe Mwenyekiti wao na wajumbe 513 wameamua ukapumzike, watu wengine uliokuwa nao chumba cha VIP wakiwa wanalia wewe ulinyanyuka ukanikumbatia kisha ukachukua simu yako ili kupongeza na kukubali matokeo kupitia ukurasa wako wa X na kuanza kujadili swala la kurudi ukumbini tayari kupokea matokeo rasmi.

Hili ni somo kubwa sana kwangu.Wewe utabakia kuwa Jenerali wangu wa kweli na kiongozi wangu siku zote. Nitakuwa tayari siku yoyote na mahala popote kutumwa au kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa.Nakutakia maisha mapya nje ya majukumu makubwa ya kisiasa.

"We protect the Purpose and not a person"
Boniface Jacob (Boni Yai)
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani
Thursaday, Jan 23, 2025.

Kwa maneno mengine Boni anaweka wazi ataendelea kuwa mtiifu kwa Mbowe, huu ni ujumbe mzito sana kwa Mwenyekiti mpya Lissu.

Lakini Boni, uliwahi kutuambia na tunaamini kwamba Mbowe anakusikiliza sana, ungempa ushauri mapema wa kujitoa kugombea wewe na yeye mngeyaepuka maumivu haya uliyotuandikia.

Hili ni andiko lenye maumivu makubwa na lawama kwa usaliti juu ya Mbowe. Boni na Mbowe mmesahau siasa ni mahesabu ya muda pia, ambapo nyie mlifeli.
 
Hii ya Boniyai ndio definition halisi ya "uchawa", sasa hivi mwenyekiti wetu mpya ni Tundu Antipas Lissu, tunatakiwa kumtii Tundu Lissu hata Mbowe anatakiwa kumtii Mwenyekiti Tundu Lissu, lakini pia tutaendelea kumuheshimu Mwamba Freeman Mbowe jabali la Siasa za Upinzani Tanzania.
 
Kura huamua mashindano,upande ulioshinda mnaungana nao mbona ni kawaida tu popote
sio rahisi kama unavyofikiria. Ndio maana viongozi wakichukua madaraka wanapanga safu ya watu wanaowaamini,, usidhani sugu, wenje, boni watamtumikia lisu kwa moyo mmoja, watamtumikia kiunafiki tu lakini rohoni wanataka afeli
 
Wakuu ujumbe wa Boni kwa boss wake wa zamani
==

Freeman Aikaeli

Mbowe Kwangu umekuwa siyo tu kiongozi wangu wa chama bali ni mwalimu, mwanafalsafa,mkufunzi,mzazi,mlezi na rafiki wa kweli. Wewe ni mfano wa kuigwaNashukuru kwa kuniamini na kunipa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kampeni zako katika uchaguzi mkuu wa chama January 2025.

Unajua,umeona, umesikia na umeshuhudia hadi sekunde ya mwisho nilivyo simama na wewe na nilivyojitoa kwa hali na mali kufanya jukumu lile zito lililokuwa mbele yetu lakini bahati haikuwa upande wetu.

Sikuwahi kufikiri au kudhani ipo siku mwalimu wangu wa siasa atanipa mimi mwanafunzi wake kazi ya kusimamia kazi yake ya siasa Hata hivyo nachezwa na machale, ninavyokufahamu itakuwa ulikuwa kuna kitu ulitaka nijifunze kwenye majukumu yangu ya kusimamia kampeni zako.

Moja ya funzo kubwa na la ajabu nitalikumbuka daima katika uchaguzi huu ni pale uliponieleza "Watu wako rasmi uliowapa jukumu la kufanya kampeni wasifanye Jambo lolote bila idhini yako, na pia katika kila jambo tutakalofanya tusikiumize chama kwa namna yoyote ile au kwa kisingizio chochote kile"Mapenzi yako kwa CHADEMA na wanachama wa CHADEMA ndiyo yalinifanya nikubali kubeba Jukumu hili zito,ulistahili "support" yangu hata kama Dunia nzima ingekusaliti kisiasa na kukugeuka bado mimi ningebakia peke yangu kuwa pembeni yako.

Ndiyo maana nilipoona kura zetu hazijatosha sikuhitaji ruhusa yako kusaini fomu ya matokeo kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu ni mshindiNa nilipokujulisha matokeo ya uchaguzi kuwa wajumbe 482 walihitaji uwe Mwenyekiti wao na wajumbe 513 wameamua ukapumzike, watu wengine uliokuwa nao chumba cha VIP wakiwa wanalia wewe ulinyanyuka ukanikumbatia kisha ukachukua simu yako ili kupongeza na kukubali matokeo kupitia ukurasa wako wa X na kuanza kujadili swala la kurudi ukumbini tayari kupokea matokeo rasmi.

Hili ni somo kubwa sana kwangu.Wewe utabakia kuwa Jenerali wangu wa kweli na kiongozi wangu siku zote. Nitakuwa tayari siku yoyote na mahala popote kutumwa au kupokea majukumu kutoka kwako hata nje ya siasa.Nakutakia maisha mapya nje ya majukumu makubwa ya kisiasa.

"We protect the Purpose and not a person"
Boniface Jacob (Boni Yai)
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani
Thursaday, Jan 23, 2025.

Maana halisi ya CHAWA PROMAX
 
Kambi zote zilizozaliwa wakati wa uchaguzi wa CHADEMA zivunjwe mara moja.

Ndugu WanaCHADEMA muogopeni kama ukoma yeyote anayehubiri mgawanyiko ndani ya Chama.

STRONGER TOGETHER
 
Akubali kuendana na mabadiliko!
Bila hivyo hatakuwa na amani.
 
Ni kweli Kwa kuongezea ni kuwa Mbowe huwa sio mbinafsi wa kumfungulia mtu dunia.

Ukiachana na siasa kina Yericko , Boni na wengineo kuna faida kubwa waliipata baada ya kuwa karibu na Mbowe .

Ikiwemo fursa za kibiashara ,network n.k.

"Walipambania mtu na sio chama"
 
Back
Top Bottom