Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Boniface Jacob: Abdul Nondo kapatikana, yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote, hata kuongea ni shida

Hatimaye kijana Nondo kapatikana muda huu,akiwa ametupwa nje ya Makao Makuu ya Ofisi za ACT.

Taarifa za awali zinasema yupo Mahututi hajiwezi kwa lolote ,hata kuongea ni shida.
===============
Kwa upande mwingine Malisa ametoa maelezo mengine kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wasamaria wema" waliomuokota Nondo Coco Beach kwanini wamempeleka ofisini badala ya hospitali? Inaelezwa Nondo amejeruhiwa vibaya na hawezi kutembea wala kuongea.

"Sasa wamempeleka ofisi za chama akafanye nini? Anyway, its a good thing kama chama kimechukua initiatives za kimkimbiza Aghakhan kwa matibabu. Kwa sasa kipaumbele kiwe afya yake kwanza, Hayo mengine tutayajua vizuri akishapona".

Soma Pia: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Source
Boniphace Jacob
Ex mayor.

View attachment 3166864
mwenye aliyeziokota zile pingu anipm tuwaloge wahusika wote wanakufwa
 
Umenifanya kuwaza marais wa awamu kadhaa nyingi hawapo tena Duniani na hivi miaka ya juzi kati karibuni walikuwepo.
Julius , Alli, Benyamini na Yoseph 🙆‍♂️🤦‍♀️😭😭
Wote wameshalala mazima 😭
Kwanini tusijitahidi kutendeana yaliyo ya haki ??
RIP all.
Mkuu ni hatari sana watu wanajisahau
 
ni muhimu sana kuzingatia uzoefu katika katika songombingo za kujiteka ili isijekuleta fedheha?

na ile taarifa ya kiongozi wa chama kwamba kijana mzoefu wa kujiteka yupo korokoroni na gari sijui la nani limebadilishwa number plate zilikua ni drama, right?🐒
W
Haya sasa mko humu kuongelea Nondo. Hivi hamuoni huu ni mchezo. Atekwe kwa lipi?

Mbona mnakuwa wazito kujumlisha na kutoa hii hesabu. Mnaacha kumuongelea Soka na Mdude mnamuwazia sijui nondo.

Hii ni daganganya toto Nanyi mmeingia box. Upinzani bongo ni sarakasi mweh

Aicitii na sisiem na sisiem ni aicitii.

Uongozi wa chama cha pande ile kurukia habari bila kuichambua. Kuna watu wanakula mkwanja kuigiza. Haya Sasa mmeambiwa kaokotwa kapele kwa ofwisi.
WE ulitakaje?
 
Ila huyu kaka anapitia mateso ktk harakati zake, si aachane tyuu na siasa zitakuja mpa matatizo makubwa zaidi au Kifo kabisa.

Namuonea huruma, [emoji25][emoji25][emoji25]
Unajua dada yangu kila mtu anaimani yake katika kile kitakachompatia ulaji na ningumu kumbadirisha mtu.

Kunawatu njia zao ni ngumu sana ila wengine ni nyepesi.
 
Hatari sana.Hivi huyu mama yetu mpendwa kizimkazi Kwanini amekuwa dikteta kiasi hiki?
 
Inasikitisha sana ,sasa wamepata faida gani? Wamemuua kibao ,wamemuua Ben saanane then?? Uchafuzi wanajipakulia minyama wao ,sasa si bora tu waendelee kufanya uchafuzi huku wananchi wakibaki salama?
Kwa nini vyama vya upinzani visifutwe tu?

Duniani tunaishi muda mfupi sana, mimi sioni faida ya kuwa mpinzani ukatekwa ukauawa au ukabaki na kilema.

Kama serikali na vyombo vya dola hawataki upinzani si ni bora watawale wao tu watu wafanye maisha mengine.

Ijulikane tu kwamba kuwa mpinzani ni jinai.
 
Sure ,wafute vyama vya upinzani wabaki peke yao ili wapinzani/wanaharakati wabaki salama.
 
Kwa nini vyama vya upinzani visifutwe tu?

Duniani tunaishi muda mfupi sana, mimi sioni faida ya kuwa mpinzani ukatekwa ukauawa au ukabaki na kilema.

Kama serikali na vyombo vya dola hawataki upinzani si ni bora watawale wao tu watu wafanye maisha mengine.

Ijulikane tu kwamba kuwa mpinzani ni jinai.
Tatizo si kuwepo kwa vyama vya upinzani. Vyama vya upinzani vinahitajika sana lakini lazima viwe kama UDP, UPDP, NLD na TLP (vyama rafiki) basi.
 
Ni dhahiri wanufaika wa huu utekaji wapo njama moja na polisi ndio maana haya matukio ya kishenzi hayakomi ktk nchi hii ya kishetani.
1000142307.jpg
 
Ninawaza sana halafu nabaki kusikitika tu.

Kwa nini binadamu anageuka na kuwa na roho ya namna hii?

ACT Wazalendo wana nini cha kutishia utawala huu hadi muwateke na kuwatesa?
Achikia mbali ACT huko mbali, Nondo ana nini cha kuitisha serikali? Kwa nn serikali inakuwa na hofu namna hii? Kuna nn?
 
Achikia mbaki ACT huko mbali, Nondo ana nini cha kuitisha serikali? Kwa nn serikali inakuwa na hofu namna hii? Kuna nn?
Kuna muda mimi ninakata tamaa, na kuna sehemu nimeposti humu kwamba ni bora upinzani waache tu, wawaachie CCM watawale..

Lakini ukifikiria vizuri, kufanya hivyo ni kuwasaliti wale ambao tayari walishatekwa na kuuawa.

Kufanya hivyo ni kumsaliti Alphonce Mawazo,

Ni kumsaliti Benard Rabiu Saanane.

Ni kumsaliti Ali Kibao na wengine wengi waliotekwa na kuuawa ama kuteswa kama akina Mdude na wengineo.

Labda, ni kuendelea tu, wote tukiuawa inakuwa ni bora zaidi.
 
Back
Top Bottom