Kweli ile nafasi ni kwaajili ya mtu mmoja tu." Kuna lugha ukianza kuongea tunajua huyu mbona sio mwenzetu, Chadema tunajuana".
" Kuna wengine wanasema liwalo na liwe tupasue mtumbwi tugawane mbao "
"Ukianza kuongea mambo yetu ya ndani kwa watu, sisi tunajua wewe sio mwenzetu, Chama hiki hakiwezi kufa kwa sababu ya mtu, anaetaka kuondoka aondoke, autuachie chama chetu"
Haya ni maneno ya Boniface Jacob, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani na kijana wa karibu wa Mbowe wakati akizindua ofisi ya chama wilaya ya Kinondoni, ambapo Freeman Mbowe alikuwa mgeni rasmi.
Yeyote atakaejaribu kuigusa tuhuma za usaliti zitamuhusu.
Lissu anavuna yale aliyopanda kipindi anawashutumu wenzie kuwa ni wasaliti kisa walikuwa na nia kama yake yakukitaka kiti kikuu.