- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Boniphace Jacob (Boni Yai) ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pwani lakini pia amewahi kuwa Meya wa Kinondoni.
Oktoba 6, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa taarifa zikieleza kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ametekwa na watu wasiojulikana hadi kufikia leo Oktoba 10, 2025 hakukuwa na taarifa yoyote kuhusu kupatikana kwake.
Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa kuwa Boniface Jacob amechapisha ujumbe kwenye mtandao wa X akisema 'Sakata la Polepole ni mradi wa kutengeneza hofu unaoratibiwa na wanaharakati uchwara nchini'
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani ujumbe ulionukuliwa ni wa kughushi kwani haujachapishwa na Boniface kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X.
Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa na Millard Ayo kama inavyoonekana. Grafiki imetumia muundo tofauti na unaotumiwa katika taarifa rasmi zinazotolewa na chanzo hicho jambo linalodhihirisha kuwa ni ya kughushi.