PostGE2025 Boniface Jacob 'Boni Yai' akamatwa na Jeshi la polisi akiwa Goba DSM

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Boniface Jacob (Boni Yai) muda mfupi uliopita leo, Jumamosi Novemba 08.2025 amekamatwa na Jeshi la Polisi Goba, jijini Dar es Salaam akiwa njiani kwenda kuripoti kituoni

Wakili Hekima Mwasipu ameithibitishia Jambo TV kuhusu kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani ambaye pia ni Meya wa zamani Manispaa za Kinondoni na Ubungo, Dar es Salaam

Itakumbukwa kuwa, usiku wa kuamkia leo Jeshi la Polisi kupitia kwa Msemaji wake lilitoa orodha ya watu 10 linaowasaka kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Jeshi hilo kutokana na matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29.2025 katika maeneo mbalimbali nchini

Katika orodha hiyo wapo viongozi waandamizi wa CHADEMA akiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa (ambaye amekamatwa na Polisi asubuhi ya leo), Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Brenda Rupia Brenda Jonas Rupia, Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Jonathan Lema, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Wakili Deogratias Mahinyila na Mjumbe wa Baraza Kuu Hilda Newton

Wengine walioko kwenye orodha hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Kada wa CHADEMA Askofu Machumu Maximilian Kadutu (Askofu Mwanamapinduzi), na Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Askofu Josephat Gwajima, ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi ilieleza kuwa inawasaka vigogo hao, lakini pia wakapewa tahadhari ya kujisalimisha kwenye Vituo vya Polisi mara moja pindi waonapo taarifa hiyo.

Pia Soma: Polisi: Gwajima, Golugwa, Brenda Rupia, Lema, Mahinyila na Mnyika wajisalimishe katika vituo vya Polisi
1762606702394.png
Chanzo: Jambo TV
 
Wamezunguuka weee wanaona kontena wawabebeshe chadema
 
It now makes sense.

Kwakuwa hawakushiriki uchaguzi nguvu nyingi walizielekeza kwenye kuuvuruga.
 
Back
Top Bottom