LGE2024 Boniface Jacob: CCM wamechagua mwisho mbaya

LGE2024 Boniface Jacob: CCM wamechagua mwisho mbaya

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
11,622
Reaction score
26,005
Jana usiku nimempigia Mzee mmoja mstaafu wa serikali aliyewahi kuhudumu kama msaidizi wa mambo ya ulinzi na usalama wakati wa Rais Julius Kambarage Nyerere.

Nimemlalamikia namna serikali ya CCM, CCM yenyewe na vyombo vya dola jinsi vilivyochezea uchaguzi wa serikali za mitaa tangu zoezi la uandikishaji,uteuzi na hata kuelekea kupiga kura na kutangaza washindi.

1.Mzee amesema kila kitu kinatokea kwa sababu,moja ya sababu ya CCM kuharibu uchaguzi ni Wananchi kukosa Imani na wa CCM kiasi cha kukosa ushawishi na kutochagulika tena .

2.Kama kuna kosa CCM watakuja Kulijutia ni Kutengeneza Mazingira ya lazima kwa Wananchi Kukosa Imani na Uchaguzi; kwa sababu Wananchi Wataiondoa CCM bila ya Kusubiri tena au Kutumia Uchaguzi

3.CCM ikiondolewa bila uchaguzi madarakani hali itakuwa mbaya sana,kwakuwa wataondolewa kwa njia ya machafuko.

4.CCM ikiondolewa kwa machafuko hawatopata nafasi ya kuendelea Kubakia na mali zao,uhuru wao na huenda hata uhai wa baadhi ya Viongozi wao au makada wao.

5.Ubaya wa Kuondolewa madarakani kwa machafuko hakutegemei muda kiasi gani kama ilivyo muda wa uchaguzi ,Mtawala anaweza Kujitangazia ushindi wa Kishindo October alafu umma ukamuondoa kwa nguvu mwezi December ili mradi Wananchi wawe wamekuchoka.

6.Kazi ya Usalama wa Taifa ilikuwa ni kama Kamisaa wa mchezo awapo uwanjani,ilikuwa ni kuangalia na Kuzuia CCM wasivuke mipaka yao katika kutawala na kubashiri hatari inayokuja mbele ili wasije kufanya Wananchi watafute njia mbadala ya Kuwaondoa madarakani nje ya uchaguzi.

Swali langu kwa Mzee likuwa Je Watanzania hawa Bongolala ndiyo wanaweza Kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu..?

Mzee amenijibu kuwa hakuna mtu mbaya Duniani kama mtu mpole na unayefikiri ni mjinga. kwa sababu siku akichukua hatua inakuwa ni "SURPRISE"

Kuna nchi zilikuwa na Wananchi wajinga kuliko hawa wa Tanzania lakini siku waliyo badilishia watawala Kibao,hakuna Jeshi lilitosha kuzuia umma wa Wananchi hao kuingia barabarani.

MAzee anaiona hali hiyo inakuja Tanzania, na wala haiko mbali sana,anafikiri pamoja na Uzee wake,lakini anaweza Kushuhudia hali hiyo kabla Mwenyezi Mungu ajachukua uhai wake.

Mzee anamalizia kwa kusema furaha ya CCM juu ya uovu huu unaoendela katika chaguzi ni ya muda mfupi sana,laiti wangejua kinachokuja mbele yao wasinge jaribu Kulivua chupi Taifa na Kulibaka hadharani kiasi hiki.

Taifa litakosa uvumilivu na kuamua kujitetea,ghazabu ya Wananchi itakuwa Juu ya CCM

Anasikitika kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kuchagua hatima yao mbaya.

20241127_095600.jpg

C&P Boniyai
 
Nikitafakari moja ya vitu ambavyo niliwahi kuvisoma kuhusu tawala mbalimbali dunia hii kwanzia huko nyuma kabisa Babeli, Mede na uajemi, wayunani, warumi na zama za kina Lenin, Hitler n.k

Ni kweli moja ya nukuu hapo "Mzee amenijibu kuwa hakuna mtu mbaya Duniani kama mtu mpole na unayefikiri ni mjinga. kwa sababu siku akichukua hatua inakuwa ni "SURPRISE". Ina ukweli mkubwa sana ila kwa watu wetu tusubiri si sasa kwasababu bado hatuna utayari.

Tujiulize tu mbona kuna wenzetu huku huku ukanda wetu wamefanya, kingine sasa hata upinzani tu wakuwapa nchi hii kwa maoni yangu lakini bado hawana uwezo wa kutusogeza walau penye kutupa unafuu.
 
Sizan labda mpaka miaka 100 ijayo,sahv bongo maisha bado ni mazuri,ukipata buku 5 unakula siku mbili

Siku watu wakikosa kabisa hela ya kula au hyo 5000 ikiwa ndogo hata kupata kilo ya mchele huwez ndipo watu wanaweza kufanya kitu ila sio sasa
 
Ni kweli moja ya nukuu hapo "Mzee amenijibu kuwa hakuna mtu mbaya Duniani kama mtu mpole na unayefikiri ni mjinga. kwa sababu siku akichukua hatua inakuwa ni "SURPRISE". Ina ukweli mkubwa sana ila kwa watu wetu tusubiri si sasa kwasababu bado hatuna utayari.
Tawala zote hizi Saba zilipitia vipindi vigumu kama CCM.

Ni dhahiri Mama anajua kabisa hakubaliki ndio maana abatumia alternative route
 
Tawala zote hizi Saba zilipitia vipindi vigumu kama CCM.

Ni dhahiri Mama anajua kabisa hakubaliki ndio maana abatumia alternative route
Ebu tafakari hivi majuzi tu nilikuta mazingira fulani kuna jamii inashangilia kwa kupewa miche ya sabuni alafu sasa nilichoumia ni mmoja tu bora basi ata box nzima.

Kuna kada inatumika sana kwenye situation za chaguzi ila hao hao siku ya mei mosi huwa wanarudi wamenuna mno baada ya wiki wanasahau.

Kuna jamii ya kufanya mabadiliko kwa sasa hapo?
 
Hahaaa.....walimu.
 
Back
Top Bottom