Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

View attachment 2828910

View attachment 2828922
View attachment 2828921
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza

3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.

4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)

5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.

5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.

6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)

7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.

8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.

9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila

10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.

Boniface Jacob EX Mayor Ubungo
We Chalamila nilikushauri uachane na hii mambo ya kushindana na nguvu za asili....angalia sasa unapata mitihani kwa damu zisizokuwa na hatia......Mwagito...upulike???
 
Hii imechoka ni balaa. Petty issue kama madada poa na kujiuza kwao nayo imekuwa ni kipaumbele kiasi cha mkuu wa mkoa kuagi a wafuatiliwe. Mtu asiye na hatia anauwawa na mkuu anaroa kejeli.
Ninkama vile nchi haina uongozi.
 
Chalamila ni mtu wa ajabu sana na sijui kwanini mama anamuamini. ni mtu anayependa kutumia mabavu, hapendi utawala wa sheria. sasa, kweli unaweza msako kuwinda machangudoa? na wakati ule alienda kuvunja vijumba vile vya wahaya, bila amri ya mahakama. sisi sote hatupendi uzinzi/umalaya, lakini huwezi kuchukua maamuzi mkononi kwenye nchi yenye sheria. anaamini hapo anapambana na machangudoa?

Kwenye mitandao ya simu amewafuata, anajua kuwa wanawake wengi wanaojiuza ni haohao wa maofisini na wanaojifanay wastaarabu, wanao uwezo kupanga wanaume hata watano kwa siku kwa njia ya simu tu, wala hajipangi barabarani. ni kweli kosa la uzururaji unaweza kuwakamata nalo na kujiuza, ila utajuaje, si kuharibu biashara za watu hiyo?

Rais kama anatusikia watanzania, na tulishamwambia, watu kama makonda, alli happy, chalamila, na yule mbunge wa misungwi hatuwataki hata kusikia wala kuwaona kwenye uongozi. sikieni maoni ya wananchi kama kikwete alivyosema.
Vijana wa mama hao. Wanatekeleza ilani chao.
 
Mtu anauza k yake wewe Chalamila inakuuma Nini dada zako umewaacha ifwagi huku inoo ifiligi fya kukinondoni vinakuhusu Nini blaza?napo waiweenda!!!maana na Yu veve pe kidomite si muunu na ludodo acha hizo mwagito
 
Hao wanawake wanaojiuza wanaipunguzia nini serikali au huyo mkuu wa mkoa??
Inashangaza kwamba mambo ya aina hii ndiyo yanakuwa kipaumbele cha hawa viongozi, kana kwamba nchi hii haina mambo ya muhimu zaidi.
Hata kufikiria tu kwa nini hawa watu inalazimu wajiingize kwenye kazi hiyo kwa ukosefu wa kazi nyingine za heshima, hilo viongozi haliwaingii akilini kabisa
 
View attachment 2828910

View attachment 2828922
View attachment 2828921
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza

3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.

4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)

5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.

5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.

6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)

7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.

8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.

9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila

10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.

Boniface Jacob EX Mayor Ubungo
Hawa wanasiasa ndio chanzo cha maisha magumu yanayosababisha vijana kujiuza kutoka na ukosefu wa ajira. Viongozi wenyewe ndio wateja wakuu wa machagudoa. Alaaniwe Chalamila na CCM yake
 
Hivi mwanamke kuvaa nguo fupi ni kujiuza?
Polisi kuweni na heshima. Isitoshe hiyo ni Night club unatarajia kuwepo na maderah!Madera!!
Je na Strip club nazo ziitweje??
Uchani upoyoyo ninyi polisi!
HILI SWALA NI PANA SANA NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA....MWANAMKE ANAYEJIUZA NA MWANAUME ANAYENUNUA WOTE SI WANAMAKOSA??? SASA KWANN ATTACK IENDE KWA WADADA TUUU?? KWANN WANAUME WANAONUNUA WASIKAMATWE PIA?.
 
Back
Top Bottom