Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Duh
 
Chalamila haamrishi [olisi, yeyre anasema sheria ifatwe, kujiuza miili yretu, iwe mwanamke au mwanamme ni kosa la jina Tanzania.


Hiyo sheria ipo toka enzi za mkoloni, hajaitunga Chalamila.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Usimtetee huyo mpumbavu. Chlamila akiambiwa hata alete ushahidi kuwa hao mabinti wanajiuza, ushahidi hana. Umewahi kusikia kuna binti yeyote au kijana wa kiume amehukumiwa jela kwa kosa la kujiuza?

Huo umegeuzwa mradi wa polisi. Huwa wanapita maeneo fulani, wanawaswaga hao mabinti, wanawatishatisha ili wawape hela, na wengine wanaenda kumalizana kwenye guest houses. Hata hao polisi ukiwauliza wamewakamata kwa kosa gani, huwa wanasema kosa la uzururaji wala siyo la kujiuza maana kumshitaki mtu kwa kosa la kujiuza lazima upeleke mahakamani ushahidi wa kuthibitisha huyo binti alikuwa anajiuza kwa nani na kwa namna gani, ushahidi ambao polisi hawajawahi kuupata. Na kama ni kahaba, alikuwa anafanya ukahaba na nani.

Kuvaa nguo fupi siyo uthibitisho wa mtu kujiuza au kuwa kahaba. Watu wanavaa mpaka mabaibui wakati wanaenda kufanya mambo yao ili wasifahamike. Hivyo mavazi siyo kigezo.

Mtu kutembea nje ya ndoa haimaanishi anajiuza au ni kahaba, bali ni kukosa maadili au kukiuka mafundisho ya dini, mambo ambayo hayasimamiwi na serikali.
 
Nimtetee mimi kuku?

Aliyeuwa, sheria itafata mkondo wake. Au huelewi hilo?
 
Tulieni tukusanye red liquid mwisho wa mwaka huu mbona mnajifanza hamjui mizim inataka juisi
 
Mkuu hapo kwenye red vipi tena? Hakuna kabila/ makabila mengine yanafanya ujasiliamali huo?!
 
Mtu aliekaa baa anakunywa unamtuhumu vipi kahaba? Bora wangekuwa wamesimama huko nje ndio wawakamate.

Tambua tanzania bado ina uhuru wa mavazi ukipanga kukamata wanawake wenye nguo fupi kila night club hapa mjini ipo hivyo.
Biashara zilizoanza hata Ukoo wake haukujulikana kama utazaliwa.
Masiaha mwenye alisafishwa nywele na Kahaba tena na mafuta ya Gharama.

Na bado Kahaba yule akawa wa kwanza kwenda kaburini kabla ya Wazee kina Petroo.

Hii ni ecosystem..ukiitingisha ndio mambo kama hayo sasa ya kuua.

Kipochi Manyoya ni cha kushikia Bastola nacho😀😀
 
Mi naona wangeua makahaba wenyewe au kuwatia vilema hao waliolaanika.
Wewe ndio mtakatifu sana?
Duniani kote watu wanapambana kuondoa adhabu ya kifo, halafu wewe unataka WATUHUMIWA wa ukahaba wauawawe?
 
Haya yote ni kutaka kuendesha mambo kama Iran kwa Ayatollah au Afghanistan kwa Taliban walipo na polisi wa maadili.
Tatizo la polisi umlaumu Chalamila?

Usikute huyo mlinzi aliwaendea na gobole lake.
 
 Hasira nilizonazo leo nadhani nisitoe kwanza salamu!



Hii nchi ina viongozi wajinga sijapata kuona duniani kote,pengine ndiyo ikawa nchi ya kwanza duniani kuongozwa na watu mbumbumbu!.

Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom,chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu eti inasemekana ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!

Baada ya lile tukio nikabaki najiuliza maswali ambayo sijapata majibu pengine labda kiongozi aliyetoa hiyo amri ya kuwafuata watu wakiwa kwenye starehe zao ndiye angenipatia majibu ya kueleweka na yenye akili timamu!.

Hivi askari mwenye akili timamu unawezaje kwenda Bar na kuingia ndani kusaka makahaba?,OK yawezekana kukawa na makahaba;ni mwanamke gani uingiapo kwenye Bar ukamkuta amevaa nguo fupi ukasema ni ukahaba?,Tangu lini kuvaa nguo fupi ukawa ukahaba?

Yaani watu waache kwenda kwenye Viwanja vya Starehe kujirusha na mabwana zao nyie wajinga mkawafuate na kuwabugudhi eti ni makahaba?

Nimewahi kusema ukahaba hauwezi kuisha na hautoisha kwa namna viongozi wanavyotaka wao!.Nchi zinazoongozwa kwa sharia za kidini bado hawajaweza kuudhibiti Ukahaba sembuse kwenye nchi ambayo haina Dini?
Yaani sasa hivi wanataka wakiingia Bar wasikute mwanamke,na wakikuta mwanamke basi awe amejifunga ushungi na kujifunika gubigubi kama wako kwenye ibada (Huu ni upumbavu wa kiwango cha juu mno)

Hamtaki wanawake wauze miili yao,Je mnataka Mikunyubenga msukumiwe nyie?

Nilidhani viongozi wangezuia biashara ya ukahaba kufanyika kwenye maeneo ya umma na kwenye makazi ya watu!,lakini kama ni Bar huko waacheni waende kwasababu ni sehemu za starehe!.

Viongozi wangekuwa na Akili nadhani wangeona ni jinsi gani ya kurasimisha hii biashara ili iweze kuliingizia Taifa kodi,pia mashirika ya kiafya yawe yanatoa semina kwa hao makahaba ili waweze kuzilinda Afya zao!.

Mkiendelea kuwafuata watu kwenye viwanja vya starehe eti kisa mnasaka ukahaba,tafsiri yake ni kwamba hao wanawake waondolewe halafu nyie mchukue nafasi zao!
 
Mhimili mkuu wa biashara ya ukahaba ni wanaume wanaonunua hao makahaba. Wakidili na wanaume hakuna kahaba duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…