Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Siyo kazi ya mwanadamu kumhukumu kahaba.Mshahara wa dhambi ni mauti,ukahaba nao ni tatizo
Hiyo kazi aachiwe Mungu mwenyewe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kazi ya mwanadamu kumhukumu kahaba.Mshahara wa dhambi ni mauti,ukahaba nao ni tatizo
DuhView attachment 2828910
View attachment 2828922
View attachment 2828921
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.
2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza
3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.
4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)
5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.
5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.
6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)
7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.
8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.
9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila
10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.
Boniface Jacob EX Mayor Ubungo
Usimtetee huyo mpumbavu. Chlamila akiambiwa hata alete ushahidi kuwa hao mabinti wanajiuza, ushahidi hana. Umewahi kusikia kuna binti yeyote au kijana wa kiume amehukumiwa jela kwa kosa la kujiuza?Chalamila haamrishi [olisi, yeyre anasema sheria ifatwe, kujiuza miili yretu, iwe mwanamke au mwanamme ni kosa la jina Tanzania.
Hiyo sheria ipo toka enzi za mkoloni, hajaitunga Chalamila.
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Nimtetee mimi kuku?Usimtetee huyo mpumbavu. Chlamila akiambiwa hata alete ushahidi kuwa hao mabinti wanajiuza, ushahidi hana. Umewahi kusikia kuna binti yeyote au kijana wa kiume amehukumiwa jela kwa kosa la kujiuza?
Huo umegeuzwa mradi wa polisi. Huwa wanapita maeneo fulani, wanawaswaga hao mabinti, wanawatishatisha ili wawape hela, na wengine wanaenda kumalizana kwenye guest houses. Hata hao polisi ukiwauliza wamewakamata kwa kosa gani, huwa wanasema kosa la uzururaji wala siyo la kujiuza maana kumshitaki mtu kwa kosa la kujiuza lazima upeleke mahakamani ushahidi wa kuthibitisha huyo binti alikuwa anajiuza kwa nani na kwa namna gani, ushahidi ambao polisi hawajawahi kuupata. Na kama ni kahaba, alikuwa anafanya ukahaba na nani.
Kuvaa nguo fupi siyo uthibitisho wa mtu kujiuza au kuwa kahaba. Watu wanavaa mpaka mabaibui wakati wanaenda kufanya mambo yao ili wasifahamike. Hivyo mavazi siyo kigezo.
Mtu kutembea nje ya ndoa haimaanishi anajiuza au ni kahaba, bali ni kukosa maadili au kukiuka mafundisho ya dini, mambo ambayo hayasimamiwi na serikali.
Mkuu hapo kwenye red vipi tena? Hakuna kabila/ makabila mengine yanafanya ujasiliamali huo?!Chalamila ni mtu wa ajabu sana na sijui kwanini mama anamuamini. ni mtu anayependa kutumia mabavu, hapendi utawala wa sheria. sasa, kweli unaweza msako kuwinda machangudoa? na wakati ule alienda kuvunja vijumba vile vya wahaya, bila amri ya mahakama. sisi sote hatupendi uzinzi/umalaya, lakini huwezi kuchukua maamuzi mkononi kwenye nchi yenye sheria. anaamini hapo anapambana na machangudoa?
Kwenye mitandao ya simu amewafuata, anajua kuwa wanawake wengi wanaojiuza ni haohao wa maofisini na wanaojifanay wastaarabu, wanao uwezo kupanga wanaume hata watano kwa siku kwa njia ya simu tu, wala hajipangi barabarani. ni kweli kosa la uzururaji unaweza kuwakamata nalo na kujiuza, ila utajuaje, si kuharibu biashara za watu hiyo?
Rais kama anatusikia watanzania, na tulishamwambia, watu kama makonda, alli happy, chalamila, na yule mbunge wa misungwi hatuwataki hata kusikia wala kuwaona kwenye uongozi. sikieni maoni ya wananchi kama kikwete alivyosema.
Kaongee vizuri na mama yako kisha urudi usome ulichoandika.Mshahara wa dhambi ni mauti, ukahaba nao ni tatizo
Kaongee vizuri na mama yako kisha urudi usome ulichoandika.Mi naona wangeua makahaba wenyewe au kuwatia vilema hao waliolaanika.
Biashara zilizoanza hata Ukoo wake haukujulikana kama utazaliwa.Mtu aliekaa baa anakunywa unamtuhumu vipi kahaba? Bora wangekuwa wamesimama huko nje ndio wawakamate.
Tambua tanzania bado ina uhuru wa mavazi ukipanga kukamata wanawake wenye nguo fupi kila night club hapa mjini ipo hivyo.
Wewe ndio mtakatifu sana?Mi naona wangeua makahaba wenyewe au kuwatia vilema hao waliolaanika.
Haya yote ni kutaka kuendesha mambo kama Iran kwa Ayatollah au Afghanistan kwa Taliban walipo na polisi wa maadili.Kujitetea kijinga huko, kwani walitumwa wakauwe walinzi?
Hamia AfghanistanMi naona wangeua makahaba wenyewe au kuwatia vilema hao waliolaanika.
Tatizo la polisi umlaumu Chalamila?Haya yote ni kutaka kuendesha mambo kama Iran kwa Ayatollah au Afghanistan kwa Taliban walipo na polisi wa maadili.
Wewe umeshaharibika sana, hata Sabaya leo akipata uongozi utageuka mtetezi wake.Tatizo la polisi umlaumu Chalamila?
Usikute huyo mlinzi aliwaendea na gobole lake.
Pokea heshima yako mama.Kujitetea kijinga huko, kwani walitumwa wakauwe walinzi?
Chalamila kaamua kupigana vita anayojua hawezi kuishinda, ni vyema akajitafakari sana pamoja na yule DC wa Kinondoni.Kama ni kweli basi kijana Chalamila atakuwa anajitia matatizoni na wabunge pamoja na mawaziri wetu maana hawa ndiyo wateja wakubwa wa madada poa.
Mhimili mkuu wa biashara ya ukahaba ni wanaume wanaonunua hao makahaba. Wakidili na wanaume hakuna kahaba duniani.