Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Huyu Chalamila kuua mtu kwake sio kitu cha kushangaza. Mara nyingi huwa anajigamba tena mbele ya waandishi wa habari kuwa anaweza kumtwanga mtu na risasi. Marumizi ya bastora kwake ndio kipa umbele kwa maamuzi atayoshindwa kuamua kwa busara.
Huyu ni mpuz cheo tu kinamlinda
Ndomana analopokalopoka alafu asipende kujifanya mwendawazim
Sanaaa.....atambue kuna watu wendawazim kuliko yeye

Ova
 
Binafsi nimezipokea taalifa za aliekua mlinzi wa bar ya Boarroom Sinza bwana Razak Anani kwamasikitiko makubwa japokua nimtu ambae hana umaarufu wowote ila nimefikilia kua mtuhuyo ni baba wafamilia kama mimi au wewe hii inamaana watoto wake na mkewake wataingia katika kipindi kigumu chamaisha yao, kikubwa zaidi nilicho jiuliza ni mlinzi alifanya nini mpaka polisi wakamfyatulia lisasi? Je si kwakuona zoezi hili nila kijinga na usumbufu kwao kwahiyo wafanye jambo litakalo zima zoezi hili nakama ndivyo hii sikama kafala?
 
Mlinzi hulinda lindo lake

Lile ni eneo lake la kazi Sasa yaweza kua kwenye kujibizana akijaribu kutetea wateja wa Bar wakammaliza yeye

Si walibeba silaha kwa hio mlinzi lazima aingilie kati na kutetea rais ingawa Askari pia ni walinzi kwa hio walinzi wamemuua mlinzi, ushaelewa
 
Nijuavyo mimi sehemu yoyote ile panapo walinzi askali wakija hua hawazuiwi kufanya shughuli zao . Hupewa talatibu za pale basi.
 
Binafsi nimezipokea taalifa za aliekua mlinzi wa bar ya Boarroom Sinza bwana Razak Anani kwamasikitiko makubwa japokua nimtu ambae hana umaarufu wowote ila nimefikilia kua mtuhuyo ni baba wafamilia kama mimi au wewe hii inamaana watoto wake na mkewake wataingia katika kipindi kigumu chamaisha yao, kikubwa zaidi nilicho jiuliza ni mlinzi alifanya nini mpaka polisi wakamfyatulia lisasi? Je si kwakuona zoezi hili nila kijinga na usumbufu kwao kwahiyo wafanye jambo litakalo zima zoezi hili nakama ndivyo hii sikama kafala?
 
Nijuavyo mimi sehemu yoyote ile panapo walinzi askali wakija hua hawazuiwi kufanya shughuli zao . Hupewa talatibu za pale basi.
Sio kweli mlinzi kazi yake ni kulinda usalama hata waje polisi maana polisi ni mlinzi kwa hio mkikutana wote ni Askari tu tofauti ni huyu ni kaajiriwa na Serekali na huyu ni mlinzi binafsi Ila wote ni walinzi na mwenye mamlaka hapo kwenye lindo husika ni huyo mlinzi aliekufa sio hao Askari walioivamia bar na kufanya mauaji, mlinzi aliekufa ana mamlaka ya kuwatimua hao Askari hadi waje na kibari cha kufanya upuuzi wao sio kuvamia tu na kuleta vurugu kwa raia hawajui sheria au PGO hawaijui?

Nb: PGO = Police General Orders
 
Police wa Tanzania bado hawajielewi, sasa hao wawili waliosababisha kifo hicho iwe ni mfano kwa kunyea debe.
 
Usha ambiwa askari walikua wame lewa
Kulewa sio kigezo cha kufanya vurugu na kufanya mauaji, hio haipo hao ni waalifu waliovaa vazi la polisi wakakutana na Askari anaejaribu kulinda usalama wa raia na Mali zao kwenye lindo lake wakamuua, itoshe kusema hivyo
 
View attachment 2828910

View attachment 2828922
View attachment 2828921
1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam.

2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza

3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa.

4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club)

5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao.

5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo.

6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu)

7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali.

8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa.

9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila

10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake.

Boniface Jacob EX Mayor Ubungo
Pia soma >>> Polisi kuua mlinzi wa bar Dar: Je, Chalamila anakwepaje kuwajibika?
Kama ni kweli basi baadhi ya viongozi nchi hii ni wa ajabu sana. Watanzania wana kero matatizo mengi (Kupanda kwa bei ya mafuta sanjali na nauli, kupanda kwa bei ya vyakula, uhaba wa mbolea, umeme, mfumuko wa bei, kukosekana kwa dolar, kikokotoo na madhara yake kwa wastaafu, na kadhalika) ambayo yanahitaji majawabu yakinifu lakini kodi ya umma leo inatumika kukamata waliovaa mini-skirt wakiwa night club na kusababisha mauaji.
 
Back
Top Bottom