Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza

Hao police na mkuu wa mkoa aliyewatuma wanatakiwa wasikilizishwe ule wimbo wa FM academia unaoitwa Heshima kwa wanawake... Siyo Kila mwanamke anayeingia bar anajiuza....... Wengine ni starehe na matumizi...
 
Kama ndivyo basi vita yote ielekezwe kwenye jeshi la police Tanzania na sio kwa mkuu wa mkoa alieteuliwa majuzi tu na soon pia atatoka na mwingine atakalia hicho kiti.


Hao wamiliki wa maeneo ya Starehe wanaoendelea kuwalipa hao Askari ujira kila usiku nao ni sehemu ya matatizo katika jamii zetu.

Maana wao ndio washiriki wa kuyakuza matatizo na yakiwazidi uwezo wa kuyatatua Kama lilivyo hili wanakuja mbele ya jamii nzima kutaka huruma na kupeleka lawama zao kwa wasiostahili.

Jamii nayo kama hivi inaingia katika mtego wa mbwa kukimbiza mkia wake mwenyewe. Ni ujinga.




Kumuita bwege kiongozi wa mkoa aliyeteuliwa na Rais wa nchi inakuongezea nini kilichokupungukia wewe?
Vita yote vielekezwe kwenye katiba, i.e. mfumo mzuri wa kuongoza. Polisi ni product tu ya mfomo mbaya. Hata wenye bar kuwalipa nayo ni tatizo la mfumo.
 
kwa sasa tunaongozwa na genge la wahuni... wanaoongoza kwa matukio machafu ni viongozi wa juu, vyombo vya mamlaka za kulinda haki.... tulitakiwa kusikia askari wako sero kupisha upelelezi, ila kila mtu yupo kimya kama kauliwa kimaa tu.. huyu mtu ana familia, kauliwa kazini akiwa anatekekeza majukumu yake, hakuwa na hatia yoyote na waliomuua hawajali... tunazingua kama nchi... huko israel raia mmoja akiuliwa serikali inatoka nje na kutoa maelezo, huku kwetu tunazikana kama panya... fu****
 
Vita yote vielekezwe kwenye katiba, i.e. mfumo mzuri wa kuongoza. Polisi ni product tu ya mfomo mbaya. Hata wenye bar kuwalipa nayo ni tatizo la mfumo.


Kwamba tukipata Katiba mpya ndio Mfumo utajijenga wenyewe?

Hii ya sasa inaruhusu hayo matendo maovu ya jeshi la police?

Wenye bar wanaungana na police waovu katika uovu wao kwa kuwalinda kwa kupeana rushwa halafu ulaumiwe Mfumo?! How?


Jamii inayoyafumbia macho matendo maovu ya wana jamii na kuanza kupapasa ardhi kwa kurunzi kutafuta mchawi ni jamii iliyoshindwa kuanzia ngazi za family mpaka Taifa.

Kwa jamii ya aina hii hata ikipata Katiba kutoka mawinguni ni kazi bure maana hata hii iliyopo sasa inakanyagwa Sawa na tambala la deki.
 
Ila hii nchi hii ukikaa vibaya unajikuta hatiani au kuuawa kabisa kisa wanasiasa.

Hawa dada poa hawawawezi.
Hiyo biashara ni ngumu mno kukomeshwa.
Au ni maagizo ya mama mbona wanakomaa sana na hii kitu.
 
Back
Top Bottom