View attachment 3031466
1.Juzi Siku ya Jumapili ya tarehe 30 Jume 2024 walifika polisi 10.
Eti akiwemo askari wa usalama barabarani (Traffic police) wanataka kumuhoji Edger Edson Mwakabela
2.Walipozuiwa kuingia wote 10 na Daktari,wakakaruhusiwa waingie japo Polisi wawili tuh.
Katika hao wawili walipo ingia kumuhoji mgonjwa
wakaona mgonjwa hawezi Kuongea,
Cha ajabu Polisi mmoja akapiga simu akiwa ndani ya chumba cha Mgojwa na haijulikani alikuwa anaongea na nani.
Maongezi yake yalikuwa ya dharau sana na kejeli lwa Mgonjwa mbele ya Daktari wake.
"Mtu mwenyewe tumemuona hapa,tunammwambia tunataka kumuhoji anajifanya hawezi kuongeaaaa."
3.Jana karudi Polisi mmoja anaitwa James ,anasema katoka Ofisi ya DCI,Dodoma (ikabidi niitwe kwa haraka sana)
Alisema amekuja kuandika maelezo ya mgonjwa.
4.Tulipo mwambia mbona mgonjwa kashaandikwa maelezo na RCO (Mkuu wa Upelelezi Polisi Mkoa wa Katavi) tangu tarehe 27 June 2024, alipokuwa Hospitali ya Mpwimbwe
5.Afande James anayedai katoka Kwa DCI,Dodoma akadai yeye kaja kuchua maelezo ya nyongeza tu.
Lakini niliposoma maelezo ambayo alikuwa ameanza kuyachukua kutoka kwa Mgonjwa, alikuwa anahoji kisa chote upya na siyo nyongeza kama alivyo dai.
6.Tukawahoji Polisi Jana kuwa wanamuhoji Edger Edson Mwakabela kama mtuhumiwa au nani..?
7.Polisi wakajibu wanamuhoji Edger Edson Mwakabela kama Shahidi katika kesi hiyo.
8.Tulipomuuliza Afande James ,Edger Edson Mwakabela anahojiwa ama Shahidi katika kesi ipi na imefunguliwa wapi..?
Kajibu hata yeye hajui kama kesi imeshafunguliwa labda tumuulize DCI.
9.Tukamuuliza Afande James,Je mapaka sasa Jeshi la Polisi limefungua Jalada la Uchunguzi/ Upelelezi sehemu yoyote..?
Akajibu hata yeye mwenyewe hajui,labda tumuulize DCI
10.Tumeshangaa sana kuona maelezo ya Shahidi yanachukuliwa kabla ya Kufunguliwa kwa Jalada la kesi au Jalada la Uchunguzi.
11.Tumekubaliana mgonjwa na mawakili wake,Jeshi la Polisi lisimsumbue tena Mgonjwa wetu
Na Hospitali ya Agakhan tumewaeleza marufuku mtu kuja kumuhoji mgonjwa bila kushrikishwa sisi au ndugu wa karibu.
12.Kama DCI alikuwa anaona Mgonjwa wetu Edger Edson Mwakabela ni Shahidi muhimu atueleze
1.kwanini Mgonjwa tulimsafirisha sisi badala ya serikali au Jeshi la Polisi kutoka katavi kuja Dar es saalam.
2. Ni kwa nini tulipoomba escort ya Jeshi la Polisi kusindikiza ambulance ya Mgonwa kutoka katavi hadi Dar es saalam tuliagizwa kuwalipa askari wawili waliomsindikiza Mgonjwa kila mmoja Tsh 300 ,000/=
Na tukalipa vizuri.
13.Mwisho,tumekataa kwa sasa,wakati huu wa matibabu Jeshi la Polisi kumsogelea Mgonjwa au chumba cha Mgonjwa wakati muhimu kama huu tunapo pambania uhai wake.
Kwa sababu wao Jeshi la Polisi ndiyo watuhumiwa namba moja waliotajwa na mgonjwa,kwamba wamehusika katika kumteka ,kumtesa na Kumpiga risasi.
Jana pia baada ya tukio hili tuliamua kumuhamisha mgonjwa kutoka wodi ya Watu wawili kwenda wodi ya chumba binafsi cha mtu mmoja ltk Hospitali ya Agakhan kwa ajili ya usalama na ulinzi wa Mgonjwa wetu.
N.B
Tutakuwa ni vichaa kama tutaendelea kuwapa Ushirikiano Jeshi la Polisi ambao ni watuhumiwa namba moja.
Tutakuwa ni wendawawazimu kama tutakubali Jeshi la Polisi lijichunguze na lijichukulie hatua ikiwa wao ndiyo watuhumiwa wa utekaji ,utesaji na mauaji.
Cc: Boniphace Jacob Meya Mstaafu