Boniyai: Profesa Kitila anadanganya kuhusu misaada ya wahisani

Boniyai: Profesa Kitila anadanganya kuhusu misaada ya wahisani

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob (Boniyai), amemtolea uvivu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, akisema kuwa madai yake kwamba nchi imejitosheleza na haihitaji misaada ya wahisani ni ujanja wa kisiasa unaolenga kuficha ukweli wa umaskini wa wananchi.

Akizungumza, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Boniyai alijibu ripoti iliyotolewa na Profesa Kitila mnamo Agosti 3, 2026. Katika ripoti hiyo, Waziri huyo alijinasibu kuwa kiwango cha misaada katika bajeti ya serikali kimeshuka kwa kasi kutoka asilimia 7.1 (mwaka 2020/21) hadi kufikia asilimia 0.9 pekee katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27.

Hata hivyo, Boniyai amepinga maelezo hayo akimtaja Profesa Kitila kama “mjanjamjanja tu” ambaye si mchumi wala mpangaji. Ameeleza kuwa masuala makubwa ya kiuchumi na bajeti yanapaswa kujadiliwa na wasomi wa uchumi, na akashutumu mfumo wa CCM wa kushindwa kutumia rasilimali watu kwa usahihi kwa kuwapa watu wasio na utaalamu kusimamia sekta nyeti, ikiwemo kumkabidhi Profesa Kitila jukumu la kusimamia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Chanzo: Jambo TV.
 
..Boni yuko sahihi.

..msaada wa wahisani unaweza kuwa sawa na bajeti iliyopangwa kwa sekta mfano ya mifugo.

..kiasi kikubwa cha bajeti kinakwenda kwenye mishahara, kuhudumia serikali, na kulipa MADENI.

..sehemu ndogo ndio inatengwa kwa shughuli za maendeleo.

..kwa hiyo ukiangalia mchango wa wafadhili, ukalinganisha na fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, utaona kwamba viongozi wetu ni wahuni kudai hawawahitaji wahisani.
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom