Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

Nimemaliza THINK AND GROW RICH cha Napoleon Hill, kwa sasa nasoma THE 7 HABITS O HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE cha Covey
Stephen Covey ni kama vile Plato wa zama hizi. Moja ya vitabu vizuri kabisa katika self improvement nimepata kusoma.
 
Reactions: Izc
where and how did you get a chance to read all these novels? did these all books help you??? how can i able to do as what you did?
 
Mwaka unaisha tena thread kama hii ifunguliwe!
 
hivyo vya religion naomba mkuu
 
Heshima yako Mkuu?.

Nianze kwa kukupa hongera za dhati sana juu ya Usomaji wa vitabu.Pili nikitie moyo juu ya Usomaji as a thinker,You discovered something interesting than anything in this world "READING".Anyone who stop reading/Learning is OLD whether at twenty or eighty.Anyone who keep reading stay young.The mostly Important things in life is to keep your mind young-Henry Ford.

Nilikuwa katika pita-pita zangu za hapa na pale nikimtafuta Muandishi Mmoja wa gazeti pendwa la miaka ya nyuma kidogo lijulikanalo kwa jina "JITAMBUE", Alikuwa akiya-publish marehemu Munga Tehenan ila baada ya kutangulia mbele za haki gazeti lake nalo likapotea.

Mlengo wangu siyo kukueleza haya yote ila katika kukupa taswira fulani tu juu ya jinsi ninavyoyatafuta maarifa yake.Katika list yako kuna kitabu cha Maisha na Mafanikio.Je ni cha Munga Tehenan?.Kama ndiyo,Je nitapata vipi kitabu kingine the same?.Kama siyo,samahani kwa usumbufu.

Naomba unisaidie kwa hili.Kumradhi.
 
Hiki cha Maisha na Mafanikio sio cha Munga. Collections ya kazi za Munga zimetengenezewa kitabu kinaitwa ''Jitambue''. Nilkinunuaga Kariakoo kwenye meza ya wauza vitabu. Ntakuangalizia kama kuna Contacts mle then ntakutumia kiongozi. Ntaku-pm my number kwa mawasilaino zaidi.
 
Kwa muda nimekuwa natamani kuwa na club kwa ajili ya watu kupata nafasi kusoma vitabu mbali mbali na taarifa mbal mbali ili kupanua uwezo na uelewa wa mambo mbali mbali katika maisha yetu. Club hii ningependa tuwekee zaid vitabu vya soft copy ili kufanya watu wengi waweze kupata nafasi ya kusoma vitabu hivyo ,pia tutatumia club hii kuweza kupeana ushauri na mbinu nzuri za usomaji wa vitabu , kuandika vitabu na pia kuuliza na kuelekezwa majina mbali mbali ya vitabu na hata wapi vinauzwa au kupatikana ( soft copy na hardcopy)

Malengo ya club hii hapa jf
1. Kupeana hamasa na kujenga/kuboresha tabia ya watu kupenda kusoma vitabu na taarifa mbali mbali
2.kuweza kupata nafasi ya vitabu mbali mbali , majina ya vitabu hivyo , na majarida mbali mbali
3. Kujenga na kupanua wigo kwa watu wengi kuweza kujifunza mambo mengi ili kupeana ujuzi kupitia vitabu
4.kupeana changamoto za kutafuta msomaji mzuri wa vitabu ( hapa vigezo vitajadiliwa na wa club ili kupata msomaji mzuri)
5. Kutakuwa na zawadi kwa msomaji mzuri wa vitabu(pia vigezo na zawadi vitajadiliwa na wana club)

Karibuni sana kwenye ulimwengu mpya wa kusoma vitabu kutokea hapa hapa JF


Binafsi ntaleta vitabu soft copy chache hapa na wengine wataendelea kuongeza vingine
 

Attachments

wewe mpaka sasa umesoma vitabu vingapi mkuu
 
Ntaomba mods wafanye marekebisho jina la Uzi nimekosea


JF CLUB MAALUM: KUSOMA VITABU NA KUONGEZA UWEZO WA AKILI NA MAARIFA
 
Sawa tunasubiri japokua humu ndani kuna uzi wa vitabu pia.
 
Wazo zuri sana mkuu! Tuombe kheri wengi waone kile unachokiona ili lengo lako litimie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…