Hahaha mimi nina madogo zangu huwa nawahasisha sana kusoma vitabu nawa motivate hata kwa kuwaambia tushindane lakini wanakwamia page ya pili.
Nikagundua ni kipaji sio kila mtu anaweza kusoma japo mtu akiwa na nia anaweza.
Yeah ni kipaji.
Mimi nilijikuta napenda kusoma vitabu tangu nikiwa mdogo kabla ya grade 1, mzee wangu nae ni mpenda kusoma vitabu.
Alikuwa na shelve kubwa la vitabu vya kila namna kwenye home library.
Hapo ndio nilisoma vitabu vayke vya James Hardley chase, vile vya James Bond, n.k.
Nilikuwa namuona anapiga miwani yake, anawasha smoking pipe, huku ana kikombe cha chai au kahawa pembeni, anasoma kitabu akiwa katulia kwenye lazy chair.
Hapendi kusumbuliwa na maswali au kitu chochote muda huo.
Nilivutiwa sana na ile hali, basi nami naingia ndani naenda kuchukua vitabu naangalia picha tu kabla sijajua kusoma.
Mpaka kufikia grade 3 nilishakuwa member wa library.
Grade 6 nilikuwa regular member wa library naitwa kutoka shule kwenda kuongea na wakaguzi na wafadhili wa elimu ambao walikuwa wanahusika na kusaidia miradi ya elimu hasa maktaba, nadhani ni Canadians wale wazungu.
Walikuwa wanachukua maoni ya member wa library.
My brothers karibu wote hakuna mtu anae pendelea kusoma sana vitabu, labda iwe kwa ajili ya kazi au shule.
Kwa mara ya kwanza bro wangu anajua kuhusu computer alisoma kwenye moja ya vitabu nilivyo azima library miaka hiyo.
Akaenda kufanya ile morning speech shuleni kwao kuhusu teknolojia ya computer na itakavyo leta mabadiliko, alionekana genius sana na kupongezwa shule nzima.
Aisee .. old memories sio mchezo!