Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Hii inahusu Wakamaria. Kuna hii kampuni mpya ya kubet inaitwa Bookee. Nilisema nijiunge nayo ili nikimbie makato ya 15% ya kodi yaliyoko SportyBet (huu nao ni wizi mwingine). Hawa Bookee kwao hukata kodi ya 10%.
Nilichokutana nacho huku Bookee ni wizi wa aina ingine lakini kwenye hiyo hiyo kodi. Yaani wao hukata 10% ya win nzima including stake yako badala ya kua 10% ya faida tu.
Mfano slip hapo juu nikiweka 100,000 kwa odds ya 1.70 (ilikua 1.698) nitapata 170,000 (au 169,830) kabla ya kukatwa kodi. Ambapo 100,000 ni mtaji wangu na 70,000 ndio faida.
Sasa hapa 10% ilitakiwa kukatwa kwenye 70,000 peke yake yaani nikatwe 7,000 kama kodi, lakini hawa wameenda kukata 10% kwenye 170,000 yote. Ina maana mtaji nao unakatwa kodi.
Huu ni utapeli, na sina uhakika kama TRA watapeleka hiyo 16,983/- iliyokatwa kwenye mapato yote, au only 6,983/- ambayo ndio napaswa kukatwa kisha 10,000/- wachikichie wao.
Haya makampuni ni kama hakuna strong regulator, sababu japokua serikali ilitangaza kushusha kodi mpaka 10% but Sportybet wao wamekomaa na 15% na hakuna anaewafanya kitu.