Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Sijui ni lugha gani nimejaribu kuangalia hata Google haijui ni lugha gani.
Hiki ni Kiswahili, na kila lugha zina lahaja. Mara nyingi huwezi kuta Kamusi imejumuisha lahaja zote za lugha fulani, sababu si jambo dogo.
 
poor daddy rich daddy
 
Ukitaka maana ya hiki kilicho andikwa nitakupa maana zake. Msomi aitwaye Abdulatif Abdallah ameelezea maana za beti hizi. Ila hakuna Kamusi rasmi inayoelezea maana ya msamiati huu.
Sio kiswahili hiko mkuu.
 
Thank you.

Nah Nowonmai, I've never read it.
Just downloaded it, I will give it a read.
Thank you for your suggestion.

I am currently enjoying The hobbit. It's just so good.

Oh, btw How's it going?

Very well dear Paula.

Glad to know that you are enjoying the hobbits.

The people(or should I say creatures?) of middle earth; hobbits, elves, Gandalf, Arathorn, even Gollum are so delightful.

Beware the Nazgul though and of course the hellish ruler of Mordor.

Can you please provide for me(and mayhaps others) softcopies of the sequels of The Fellowship of The Rings? To wit, The Twin Towers and The Return of the King? I have read them before of course but I couldn’t keep the copies and as you are testifying, the Middle Earth is unforgottable.

My blessings.
 
1. Dafina ya Umalenga
2. Mtango wa Kiswahili
3. Upisho wa Umalenga
4. Kale ya Washairi wa Pemba (Kamange na Sarahani)
5. Utenzi wa al Inkishafi

Vitabu hazina kubwa ajabu, naendelea kusoma.

Naendelea....

Mkuu, hongera sana kwa kuwa na hivyo vitabu.

Riwaya, tamthiliya na mashairi ya kiswahili ni tamu sana.

Ni miaka sasa toka nisome Mzimu wa Watu wa Kale, Kisima cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Kiu, Nyota ya Rehema, na takribani utunzi wote wa Shaaban Roberts lakini mpaka sasa sijawasahau bwana Ali, Kipwerere, Bwana Msa, Najum, Kassim Hakimu Marjani, Bi Selume, Mwinyi, Iddi, Rehema, Fouad na Utubora Mkulima kwa uchache.

Binafsi nakumbwa na hali ambapo kupata vitabu vya kiswahili ni ngumu zaidi kuliko vya kiingereza.

Nitafurahia sana kusoma vitabu vya kiswahili vya maudhui yoyote vitakavyoletwa humu.
 
Safi kabisa, ila mimi kuna vitabu huwa siwezi kuvisoma kwani huwa naona bapoteza muda hasa vitabu vya Riwaya na Tamthiliya huwa siwezi kuvisoma viwe vya lugha yoyote ile.

Nakipenda sana Kiswahili.
 
Kimakwe ni baada na kwisa ni maliza.
Naam kiswahili hasa ni baada na sio kimakwe.

Na kiswahili hasa maliza,au kumaliza na sio kwisa kama ulivyoeleza.

Kwisa sio kiswahili na kimakwe sio kiswahili.
Ni Kiswahili cha lini hiki ?
Kama sio cha kale basi min baabi awlaa kisiwe cha kisasa.
Unaujua Utenzi wa al Inkishafi ? Uliandikwa lini huu Utenzi ?
Siujui na hata hilo neno inkishafi sio kiswahili asili yake
 
Naam kiswahili hasa ni baada na sio kimakwe.

Na kiswahili hasa maliza,au kumaliza na sio kwisa kama ulivyoeleza.

Kwisa sio kiswahili na kimakwe sio kiswahili.
Kijana mbona unabisha vitu usivyo vijua. Niambie sasa hiko ni lugha gani ?

Maneno mangapi ya Kiswahili yana maana kwa Kiswahili ?

Niambie sasa Kwisa ni lugha gani na Kimakwe ni lugha gani ?
Siujui na hata hilo neno inkishafi sio kiswahili asili yake
Sasa kama huujui kwanini unapinga tena bila elimu ?

Tamko ni la asili ya Kiarabu ila ni la Kiswahili sababu limechukuliwa huko. Kwahiyo lina baki kuwa ni Kiswahili ila ni tamko la asili ya Kiarabu.
Kama sio cha kale basi min baabi awlaa kisiwe cha kisasa.
Jibu nilicho kuuliza.
 
Kijana mbona unabisha vitu usivyo vijua. Niambie sasa hiko ni lugha gani ?
Dah kwa hiyo kama lugha yake haifahamiki ndio ipachikwe kuwa lugha yake kiswahili ?

Kutokujua kwa lugha yake haijawa hoja ya kuwa hiko ni kiswahili,yaani neno combigenouz nikikataa kama sio kiswahili haina maana kuwa najua lugha yake.


Maneno mangapi ya Kiswahili yana maana kwa Kiswahili ?
Yapo Mengi tu yenye maana kwa kiswahili lakini sio hayo uliyoyataja,mengine yapo ila sio kwa hayo uliyoyataja.

Sawa mengine yapo yenye maana kwa kiswahili lakini je kuwepo kwa mengine ndo hoja hiyo ?

Tena yapo lakini sio kwa utofauti huo ambao upo katika hayo maneno yako wewe.


Tamko ni la asili ya Kiarabu ila ni la Kiswahili sababu limechukuliwa huko. Kwahiyo lina baki kuwa ni Kiswahili ila ni tamko la asili ya Kiarabu.
Tunakubaliana kuwa inkishafi sio neno la asili la kiswahili kama nilivyosema huko juu,


Jibu nilicho kuuliza.
Nimekujibu labda hujaelewa.

Nasema kwamba kama sio kiswahili cha kale basi hakiwezi kuwa kiswahili cha sasa hata kidogo.

Kwa hiyo sio kiswahili asili yake.
 
Dah kwa hiyo kama lugha yake haifahamiki ndio ipachikwe kuwa lugha yake kiswahili ?

Kutokujua kwa lugha yake haijawa hoja ya kuwa hiko ni kiswahili,yaani neno combigenouz nikikataa kama sio kiswahili haina maana kuwa najua lugha yake.
Unapo kanusha kitu kitu hakikisha una ushahidi dhidi yake. Huwezi kusema hiki si Kiswahili kisha unashindwa kuthibitisha ya kuwa si Kiswahili.


Sasa thibitisha ya kuwa Kimakwe na kwisa si Kiswahili.

Unaandika kama unajua unachokiandika ila unashindwa kuthibitisha. Wewe niambie tu umejuaje kwamba hicho si Kiswahili.
Tunakubaliana kuwa inkishafi sio neno la asili la kiswahili kama nilivyosema
Ni neno la Kiswahili ila lina asili ya Kiarabu, la lilivyo tamko "Baada" ambalo huko juu ulisema ni Kiswahili hasa, ila lina asili ya Kiarabu. Kwahiyo Inkishafi ni Kiswahiki chenye asili ya Kiarabu kadhalika tamko "Baada" ni Kiseahili ila lenye asili ya Kiarabu.
Nimekujibu labda hujaelewa.

Nasema kwamba kama sio kiswahili cha kale basi hakiwezi kuwa kiswahili cha sasa hata kidogo.

Kwa hiyo sio kiswahili asili yake.
Ndiyo maana nilikwambia hujajibu swali. Kuna kiswahili cha Kale na Kiswahili sanifu, hakuna Kiswahili cha kisasa mzee. Kiswahili ni sarufi na fasihi na mengineyo. Weka akilini hili.

Sasa kama siyo Kiswahili ndiyo utuambie ni nini hiki ? Au unafikiri mambo yanatokea tu pasi na asili au kinyume chake. ?
 
Sawa mkuu sina hoja nilikurupuka haswa.

Sina usahihi katika hili
 


Tafuta hicho kitabu usome kina Tendi Tatu za Kale ambazo ni :

1. Utendi wa Fumo Liyongo
2. Utenzi wa Inkishafi
3. Utendi wa Mwanakupona

Nakuonyesha ya kuwa hicho ni Kiswahili. Siku nyingine uache kukurupuka na kusumbua watu.
 

Attachments

  • IMG_20200926_213107.jpg
    200.6 KB · Views: 21
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…