Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Kwa hilo ondoa shaka,sote jambo tuta share
kwa lile ninalotaka, napaswa kulipupia
Yanichukua miaka, hili jambo kufikia
Ewe paula mpendwa, ngoja wangu mrejesho.
Okay
Hivi kinapatikana kwa soft ama hardcopy?
 
Title yake, East of Eden imetoka katika kitabu cha Mwanzo 4:16.
na moja ya maudhui yake ni uhuru wa binadamu kuitawala dhambi( Mwanzo 4:7).

............................. ...Nitarudi.
Nilikua natafuta kitu kama hiki, Sometimes I like to read bible stories outside the bible. Tuakusubiri kwa kweli urudi tu.
 
Wengine wanasema kina udini ila mimi naona sio.
Labda tuwaulize Nowonmai na Kiranga wao wamekiona namna gani.
Hakina udini.

Na hata hizo zinazoitwa dini pia ni hadithi tu.

Kwa hivyo, mimi sioni msingi wa kukataa kitabu kwa sababu ni cha kidini.

Kwa sababu, hata vitabu kama kwa mfano, Biblia, ukiichambua kwa undani kwa kumsoma mtu kama Dr. James Kugel katika "How To Read The Bible", utaona vitabu vya dini pia ni hadithi za kutungwa na watu katika kupambana na maisha yao ya kila siku.
 
Paula Paul umefuatilia series ya Hemingway PBS?

Very interesting. I bought the accompanying book yesterday.







 
Yeah, hata mimi nimeona hivo. Kwa sababu hata habari za Cain na Abel zilihadithiwa tu kwa kuonekana kama Aron na Cal wanakaribia kisa hicho.
Ni sawa sasa hivi mtu apatwe jambo tufananishe na kwenye Bible mtu alitokewa na jambo hilo.

Nimetamani kusoma hiyo "How To Read The Bible "

Cc Pendael24
 
Hapana sijafuatilia kabisa.
Asante kwa link. Ipi inapaswa kuanza?

Edit: Nimeona

 
Hapana sijafuatilia kabisa.
Asante kwa link. Ipi inapaswa kuanza?

Edit: Nimeona

View attachment 1750521

Hi. Paula, naomba unisaidie link ninayoweza kupata free pdf. Hata hivyo kama wewe au wengine wanaweza nisaidia vitabu kama:
1: The Laws of Human Nature- Robert Green
2: Dark Psychology Series books
- Hapa kuna mlolongo wa muendelezo wa zaidi ya kitabu kimoja.

Asante.
 
Hi, HS CODE.
Here you go ,utapata kwa formats mbalimbali.
Give it a shot.
 
Ni kweli vitabu vya dini vimetokana na hadithi, na kila hadhithi Ina mazingira yake kwa muwasilishaji na anaewasilishiwa.
Sisi wengine tulio zipokea hizo hadithi zimetufunga katika kitu kinaitwa imani.
Kiasi ambacho usingependa kusikia maelezo mengine yanayo husu hadithi ulizozipokea hapo kabla kutoka katika chanzo kingine.


Kwa Mimi binafsi natamani sana kusoma hadithi zinazopatikana kwenye biblia nje ya biblia yenyewe Kama hiko kitabu tunachokielezea.
 
Nimemuelewa na kuelewa Paula, kazi kwangu ni kukitafuta Kama kinapatikana kwa wepesi.[emoji120][emoji120]
 
Sawa nasubiri urudi kwa hitimisho.

Samahani kwa kukawia Paula na Pendael24.

Kwenye edition ya kwanza(1952), mwandishi alitoa utangulizi ambao nadhani twaweza sema ndiyo malengo yake kwa huu utunzi.



Kama tunavyoona hapo, moja ya dhana alizotaka kuwasilisha mwandishi ni wema na uovu.

Dhana ya wema na uovu ni ya zamani zaidi kuliko dini tunazo practice wakati huu na hivyo kwa maoni yangu East of Eden hakina udini ndani yake licha ya kuwa na maudhui kadhaa ya kibiblia.

Angalia namna mwandishi anavyotumia irony kufikisha ujumbe:-

Lee na wasomi wa kichina wanaibua suluhisho linalokubalika toka biblia ya kiibrania.

Cathy/Kate hatimaye anampenda sana mmoja wa watoto wake aliowatelekeza wakiwa wachanga na kumwachia urithi wa mali ingawa hakubadilika kabisa katika aspects zake nyingine za uovu.

Charles pia anabadilika ukubwani na kuweza kuishi kwa amani na Adam baada ya kuwa na chuki kali sana dhidi ya huyu ndugu yake.

Angalia pia jinsi familia ya Samuel Hamilton ilivyojaa contradictions.

Kwangu mimi basi hiki kitabu kina maudhui mengi lakini sio hilo la udini au kama lipo sio la muhimu sana.

BTW Kuna mahali mwandishi analinganisha ujio wa waeneza dini na makahaba mjini na ni kama vile wote wana ushawishi sawa au pengine ushawishi wa makahaba una uzito kuliko ule wa wainjilisti!

Don’t know why I feel so much at loss after writing this.

Paula and others please let me have your views.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…