My LIfe, My Purpose,
because it is such a funny, fictitious comedy!
Mkapa aliitwa "Mr. Clean". Kama sifa ya kuwa mpinga rushwa.
Alipopata urais tu, Kitwana Kondo akataka kuonana naye ili ampongeze.
Mkapa akamwambia, kama pongezi, chukua ukurasa wa gazeti la serikali uchapishe gazetini. Such a journalist!
Ujumbe ulikuwa kwamba hataki watu wamzonge ili kutafuta influence.
Hapo hapo, rafiki yake Mkapa, "Sir" Andy Chande akamnunulia Mkapa Range Rover Vogue kama pongezi za kuwa rais.
Mkapa akalichukua, aka park pale Sea View.
Nikasema Mr. Clean kakubali hii pongezi ya Range Rover Vogue kutoka kwa Andy Chande wakati Kitwana Kondo hata kukutana naye tu kakataa?
Nikasema labda atalirudisha. Ikawa kila nikienda Sea View nalikuta.
Kutoka hapo nikajua kwamba habari za "Mr. Clean" ni mazingaombwe tu.
Ukijua habari kama hizi, ambazo kuandikwa kwenye vitabu sitegemei, utajua hivi vitabu ni public relations campaign tu.