Nowonmai
JF-Expert Member
- Jan 15, 2019
- 1,050
- 1,126
Sina ufafanuzi ninaodhani unaoweza kukusaidia
Ila ninachofahamu kwa uhakika ni kwamba unaoitwa mwili ni mkusanyo wa taarifa nyingi za watu waliopata kuishi miaka mingi huko nyuma
Waliopata kushughulika na changamoto nyingi na kuzipatia utatuzi iwe mahusiano, kiafya, kiuchumi, kiutawala n.k
Lakini vyote kwa ujumla vimekusanywa kwenye mwili mpya mmoja ambao ni wewe..!
Kwa ufupi ni kwamba hujawahi kufa na wewe ni majibu ya wale waliokutangulia.. kila changamoto na majibu yake vipo ndani yako
Sisi wengine kwako ni ukumbusho tu na si lolote, tungependa sana kuelewa pia ulimwengu ulio ndani yako tunapopata mda na sisi tupate kukumbuka mengi
Lakini cha kusikitisha dunia sasa hairusu hilo tumekuwa ni wakulishwa kila aina ya chakula na kuamuliwa namna ya kufikiri.!
Asante mkuu ManchoG kwa hii tafakuri.