Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

There!!!
I think you are amazing.

I think you are too. More than amazing I ‘d say.

Hey, ever come across Masha Hamilton’s The Camel Bookmobile?

If not hasten to find and give it a glance.

I am sure it will be worth the time that you will spend going through it.
 
Kuna aliye na kitabu cha Relationship Goals by Michael Todd maana nasumbuliwa na mtu mpaka basi 😄
 
I think you are too. More than amazing I ‘d say.

Hey, ever come across Masha Hamilton’s The Camel Bookmobile?

If not hasten to find and give it a glance.

I am sure it will be worth the time that you will spend going through it.
Thank you.

Nah Nowonmai, I've never read it.
Just downloaded it, I will give it a read.
Thank you for your suggestion.

I am currently enjoying The hobbit. It's just so good.

Oh, btw How's it going?
 
1. Dafina ya Umalenga
2. Mtango wa Kiswahili
3. Upisho wa Umalenga
4. Kale ya Washairi wa Pemba (Kamange na Sarahani)
5. Utenzi wa al Inkishafi

Vitabu hazina kubwa ajabu, naendelea kusoma.

Naendelea....
 
Okay kwahiyo huku ndi unajifunza kiswahili kigumu Zurri?
Mathalani ukisoma katika "Utenzi wa al Inkishafi" utakutana na ubeti huu wa sita (6). Nanukuu :

  1. Kimakwe kwisa kuzikamili,
himdi na sala kuziratili,

Niyadhihirishe yangu makali,

ambayo moyoni nikusudiye.

Hiki ni Kiswahili cha kale.
 
Okay kwahiyo huku ndi unajifunza kiswahili kigumu Zurri?
Ukirudi katika kitabu "Mtango wa Kiswahili" unakutana na ubeti huu :

Kisi kisi kisikule, Kisi hakikisi kisi
Kisi sikia si kile, Kikanitusha na isi
Kisi lesso kifungile, chendapo kisi kihisi
Kisi hakikisi kisi, kisi leso kisikule
 
Nimecheka kidogo unaweza sema ni Kiswahili kigumu ila ni kiswahili cha kale ambacho ni kitamu ila walio wengi hawashughuliki nacho.

Naweza pia sema hapana huku najifunza ufasaha wa Kiswahili na utamu wake.
Lakini kiswahili cha "kale" wengi hawakielewi enh? Wewe unakitumia kuongea na nani?
Haukutani na maswali ya "sijaelewa " mengi?
 
Lakini kiswahili cha "kale" wengi hawakielewi enh? Wewe unakitumia kuongea na nani?
Haukutani na maswali ya "sijaelewa " mengi?
Sikutani na maswali hayo, sababu najua kuongea kulingana na muktadha wa hali.

Soma beti hizi katika Shairi la 19 ubeti wa 1 na wa 5, katika kitabu "Upisho wa Umalenga" cha Mwalimu Hassan Mbega,anasema :

1. Achani maneno hayo, tena achani kabisa Achani muyanenayo, kudhani pendo ni pesa
Si pendo hilo ni payo, si pendo ni payo hasa Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa

5. Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa
Pendo lenye jakamoyo, na tamaa ya mapesa
Pendo la namna hiyo, ni wapi liliko hasa?
Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa

Kwa leo tosheka na vitamu hivi.
 
Mathalani ukisoma katika "Utenzi wa al Inkishafi" utakutana na ubeti huu wa sita (6). Nanukuu :

  1. Kimakwe kwisa kuzikamili,
himdi na sala kuziratili,

Niyadhihirishe yangu makali,

ambayo moyoni nikusudiye.

Hiki ni Kiswahili cha kale.
Unatumia kamusi gani? Naweza kuipata?
 
Ukirudi katika kitabu "Mtango wa Kiswahili" unakutana na ubeti huu :

Kisi kisi kisikule, Kisi hakikisi kisi
Kisi sikia si kile, Kikanitusha na isi
Kisi lesso kifungile, chendapo kisi kihisi
Kisi hakikisi kisi, kisi leso kisikule
Unanidanganya hiki sio kiswahili.
 
Unatumia kamusi gani? Naweza kuipata?
Ukitaka maana ya hiki kilicho andikwa nitakupa maana zake. Msomi aitwaye Abdulatif Abdallah ameelezea maana za beti hizi. Ila hakuna Kamusi rasmi inayoelezea maana ya msamiati huu.
 
Sikutani na maswali hayo, sababu najua kuongea kulingana na muktadha wa hali.

Soma beti hizi katika Shairi la 19 ubeti wa 1 na wa 5, katika kitabu "Upisho wa Umalenga" cha Mwalimu Hassan Mbega,anasema :

1. Achani maneno hayo, tena achani kabisa Achani muyanenayo, kudhani pendo ni pesa Si pendo hilo ni payo, si pendo ni payo hasa Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa

5. Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa
Pendo lenye jakamoyo, na tamaa ya mapesa
Pendo la namna hiyo, ni wapi liliko hasa?
Viwili katika moyo, kuviweka vyanitasa

Kwa leo tosheka na vitamu hivi.
Nimetosheka lakini natamani kujua maana zake.
Ulisema unaandika mashairi. Naweza kuona shairi lako moja?
 
Back
Top Bottom