Kweli siyo kirahisi, pengine ndiyo maana imenichukua muda mrefu kukianza. Mtu mmoja au sehemu moja inaweza kuwa na majina kibao kulingana na contexts. Na kila kitu kina jina, kuanzia pete, panga tarumbeta nk. Na si majina rahisi kwa sisi wabantu. Sisi na Dagor Bragollach wapi na wapi!!😀😀. Hii ni kaz complex sana, hadi lugha mpya iliundwa!!! Ila niko full nondo, nina map na narejea mtandaoni. Bila kucheki map kwa makini hiki kitabu ni ngumu kukielewa. Lakini mpaka hapa nimekienjoy sana na napendekeza kwa wapenzi wa high fantasy wakisome.
Nilisoma The Hobbit kabla movies zake hazijatoka, kazi nzuri na movies zake nzuri pia. LoTR sidhani kama nitavisoma sababu nilianza na movies zake.
Heshima kubwa kwa Tolkien.