Hapa mimi mtoto wa kabwela natumia 3500 kwa cku,na maisha yanasogea
Unasoma Chuo Gani? Unapotoa Comment juu ya hili ujue kuna wenzio baadhi ya vyuo wanalipa nauli kwenda Chuo,na Gharama ya Hostel @day 1000/= hebu toa mchanganuo wako tuone daily expenditure yako.
Ya wenzio ipo hivi....
Kwa maisha ya kati, si ya juu wala ya Chini .
MATUMIZI YA LAZIMA
1)Breakfast 800/= Baadhi ya Vyuo 500/= inatosha.
2)Lunch 1500/= Baadhi ya Vyuo 1000/= inatosha ila tunachukua average cost vyuo vyote.
3)Dinner 1500/=
4)Maji ya kunywa kilimanjaro 1.5 litre 1500/=
5)Room 1000/=
6)Usafiri To and fro 800/=
JUMLA 7100/=
MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA(Tujue kua Nyumbani hupati chochote(Watoto wa wakulima) hivyo unategemea hiyo pesa kwa kila kitu)
7)Mawasiliano 500/=
8)internet 500/= Hapa unajiunga na Cheka.
JUMLA 1000/=
JUMLA KUU 7100+1000=8100.
Hapo bado hujanunua Nguo,hujatoa sadaka kanisani,hujamsaidia mdogo wako nyumbani maana anajua upo Chuo kikuu Mnapewa Pesa,Hujatenga Nauli ya Kurudi Nyumbani wakati wa Rikizo,hujatoa nauli ya kwenda Town kupata mahtaji mawili matatu.
NOTE: Hata tukisema Pesa ya Loanboard ni kwa ajili ya Kukusaidia ukiwa Chuo Tu,Lakini kiuhalisia kwa Maisha ya Watanzania haya Matumizi niliyoyaanisha hapo juu kama Matumizi yasiyo ya Lazima ni Lazima utakabiliana nayo Maana Nyumbani Wanajua Chuo Mnapata Pesa,so ata ukiomba Hupewi na Wengine nyumbani hawana Msaada Kabisa Hata Sekondarai Ada ilikua ya Kuungaunga.