KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Leo nimebahatika kupita katika Kivuko cha Kigongo - Busisi Mkoani Mwanza, nikiwa abiria nimekuta hali ni mbaya, ni kero Kwa kila mtu.
Foleni ya magari ni kubwa sana, foleni ya abiria ni kubwa, abiria unatumia takribani saa mbili hadi tatu kuvuka, magari yanatumia saa mawili hadi tatu pia kuvuka kwenda upande wa pili.
Nimeona kuna vivuko viwili tu ndivyo vinafanya kazi. Pande zote mbili za kivuko ni hatari, foleni kubwa mno, magari ni mengi, hali hii inachosha sana kwetu abiria, hatujui tatizo ni nini, je ni uchache wa Vivuko au kuna shida kwenye uongozi?
Leo saa kumi na mbili tufika hapa kivukoni, lakini tumekuta magari ya toka jana yake bado hayajavuka, tumefanikiwa kuvuka saa tatu kamili, tumechoka sana.
Abiria wanakaa kwenye lile jumba la abiria hadi wanachoka, changamoto inaonekana vivuko ni vichache na mahitaji ni makubwa.
Vivuko ni kama vimelemewa, na kasi ya hivi vilivyopo inaonekana ni ndogo, Serikali iingilie kati hii hali ya Kigongo - Busisi, inatukera sana abiria, inatukera sana wananchi.
Nimeangalia pande zote mbili za vivuko, nimekuta foleni kubwa na ndefu ya magari Tena magari ya abiria, foleni inafika hadi mlimani kwenye Barabara Kuu, unakuta foleni Hadi kilometa moja urefu wake.
Watu tunachoka, inakera na kuleta hasara kwetu wananchi, maana muda ni mali.
Serikali ifungue Daraja la Magufuli watu tupite hii hali ya kivuko inatuchosha sana.
Pia soma:
~ Mwanza: Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) umefikia 96.3%
~ Rais Samia akagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli, ujenzi wafikia 93%
~ Baada ya kivuko Busisi kuzingua, wananchi waruhusiwa kupitia katika Daraja la Magufuli na kuvuka kwa mguu hadi ng’ambo
~ Vivuko vya Kigongo-Busisi havifanyi kazi leo. Daraja lifunguliwe kwa dharura kuruhusu magari