Bora Dkt. Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge - Dr Kikwete 2010

Bora Dkt. Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge - Dr Kikwete 2010

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Hii ni kauli isiyosahaulika toka Kwa Mwenyekiti wa 4 wa CCM na Rais wa awamu ya 4 wa Tanzania Dr Jakaya Mwisho Kikwete aliyoitoa mwaka 2010 kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huo.

Alitoa kauli hiyo kuonyesha Jinsi ilivyo ngumu kudeal na Tundu Lissu kama kiongozi mpinzani kuliko yeyote akiwemo Dr Wilbroad Slaa. Kwa maana halisi Dr Kikwete alikuwa tayari kupoteza Utais na kubaki Mwenyekiti wa Chama chake Taifa kuliko kuongoza serikali itakayokosolewa Bungeni na na nje ya Bunge na Mh.Tundu Antipus Mugwayi Lissu.

Kinachotushangaza wengi Kwa Sasa eti kuna wanaCCM wanaombea Tundu Lissu huyo huyo awe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Freeman Aikael Mbowe.

Naamini Wapinzani ndo walipaswa kushabikia hili na si wanaCCM, lakini Kwa vile wamepofuka na wako tayari kushabikia chochote kuhalalisha posho haramu wanazolipwa kuchafua mitandaoni, tuseme Acha Lissu aje, na wote tuseme "AMINA".​
 
Lissu afungue chama chake cha wanaharakat ambapo atapata sapoti ya wanaharakat na diaspora wote
 
Back
Top Bottom