Bora Hayati Dkt. Magufuli, haya yamerudi tena!

Bora Hayati Dkt. Magufuli, haya yamerudi tena!

Mpuuzi kweli wewe. Huna jipya kazi yako kuja na utoto jukwaani alafu hujui hata kuandika huna shule kichwani. Hao maelfu ya watu walio uwawa uliwaona? Kutwa unakomenti upuuzi wa kikobazi.
Ni kwa sababu hakuna ulichopoteza kwenye uvamizi. Mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi.

Mambo yangu ni ya kitoto , mtaendelea kuyapata hayo mambo ya kijiutuzima kwa kuja kulalamika JF .

Kumbuka karma itaendelea kuwatafuna mpaka mtapojutia mliyoyafanya na kuomba radhi.

Dua ya mwenye kudhulumiwa hairudi
 
Mpuuzi kweli wewe. Huna jipya kazi yako kuja na utoto jukwaani alafu hujui hata kuandika huna shule kichwani. Hao maelfu ya watu walio uwawa uliwaona? Kutwa unakomenti upuuzi wa kikobazi.
Nakusaidia kumshangaa.

Anachanganya dini na siasa. Hawa jamaa dini mbele ya kila kitu kama vile Znz ni Theocratic badala ya Democratic.

Anasema Nyerere aliuwa anasahau kupitia dini yake hiyo Sultan Jamshid alikuwa akipasua mimba (kikatili) za Watumbatu hadharani kweupe ili watoto wake waone mtoto anavyolala tumboni alafu anatupa mizoga ya maiti!

Anasahau kwamba Ikulu ya Znz nguzo zake zimeshikiliwa na maiti za Wakojani, Wangazija na Wanyamwezi waliofukiwa humo kwa zege!? Karma itaanza na wao Mahizbu Mawakala wa Sultani.

Hayo hapo juu pia Nyerere ndiyo aliyafanya au alileta mapinduzi kuyatokomeza?

Huyo Hizbu anataka wangeendelea kuwa chini ya utawala dhalimu wa Sultani?

Nchi inalipiwa hata bili ya umeme na bara! Bajeti yake sawa na bajeti ya Azam FC! Alafu hawana shukurani! Mshukuruni Magufuli kuwapa Dr. Mwinyi ili awanyooshe mpate maendeleo.

TRA ikikusanya pesa zinatumika hadi kwao Znz wakati ZRA ikikusanya mapato hakuna mgawo unaoletwa bara, Baghosha!
 
Magazeti dada mawili ya The Citizen na Mwananchi yameripoti ukwepaji kodi wa kupindukia (Tzs.3.3 tr) huku tukikuza deni la taifa kwa kukopa hadi Mhimili wa Bunge unastuka. Magazeti haya yamejizolea sifa lukuki kwa uandishi wenye weledi.

Kauli ya Rais ni Sheria

Kaulimbiu ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake inaligharimu taifa na kuleta madaraja ya maisha (stations or life) yanayostawisha matabaka kwenye jamii.

Hivi sasa watu wanakula mlo mmoja maana unga umetinga 2000/ kg, maharagwe 4000/ kg, mchele wa gredi ya chini 3000/ kg, sukari tangu enzi ya Dr. Omar VP imeshinda awamu zote 4 kushusha bei.

Mafuta ya kula hivi sasa ni anasa, watu wanakula chukuchuku kwenye nchi inayolima mawese, pamba, mahindi, karanga, minazi, ina samaki na wanyama vyote hivyo vinatoa mafuta ya kula.

Nchi inaenda kwenye uchaguzi bila agenda. Vyama havina agenda ilhali wananchi wana agenda ambayo vyama haviioni.

Haiyumkiniki kwamba hata miradi ya kimkakati ya maendeleo imekwama kumalizika kuelekea 2025 licha ya ela iliyokopwa Tzs.42 tr ni zaidi ya thamani-jumla ya miradi yote mikubwa.

Znz kuna paa hadi umeme wanaopewa hauwatoshi wamelazimika kuomba waongezewe kiwango cha umeme.

Znz hiyo hiyo bei ya bidhaa na huduma zimebaki kuwa himilivu wkt bara uwezo wa mlaji kununua (purchasing power) umeanguka hadi kula mlo mmoja. Znz na Tz Bara ni nchi moja.

View attachment 2518066View attachment 2518067
Chifu anashindana kunya tu pale magogoni hakuna cha ziada
 
Kenya wamefanya uchunguzi wamegundua mizigo inayotoka China ni mingi ila inayolipiwa kodi ni michache
 
Back
Top Bottom