Bora Matumizi ya Projector badala ya TV kuangalizia movie

Bora Matumizi ya Projector badala ya TV kuangalizia movie

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Wadau kutokana na kuwahi ibiwa Tv zangu za Samsung mara 3 nyakati tofauti tofaut sasa nmeamua kuachana na kununua TV.

Sasa nawaza kununua Projector. Naomba ushauri kwa projector ya kufaa kwa ajili ya kuangalizia movie. Nahitaji Full HD, iwe 4K, 3D ,High Resolution.

But katika hayo yote naomba wataalamu mtufafanulie vizuri. Tukianzia na hilo wazo la kununua projector badala ya TV. sabab projector ni mobile so ntaweza ihamisha isiwe inalala Sebuleni.

But pia nimeona EBAY wakiuza projectors mpaka kwa usd 100 na zipo za chini ya hiyo Usd 100. Walio na uzoefu wa kuagiza mizigo Ebay wanipe ushauri pia.

Nawakaribisha wataamu akiwepo Chief-Mkwawa
 
Projector hazina picture quality nzuri kma TV. Projector ya laki 8 inaweza kuwa na picture quality kama ya TV ya laki 3. Imarisha ulinzi tu nyumbani kwako
 
Projector native 4k bei zake ndefu sana halafu haiwezi kuwa full HD na 4k hapohapo. Nyingi bei zake ni milioni 3 kupanda.

Kwa budget zetu za kitanzania HD ama Full HD projector ina make sense zaidi.

Angalia tu eneo lako, umbali wa unapotaka kuiwekea hadi ukuta ulipo, mwanga etc.
 
Kama unaweza kuibeba projector na kuingia nayo chumbani,kinakushinda nini kuibeba hiyo TV yako wakati TV nyingi za kisasa zinabebeka kirahisi! au kama TV zako ni model za zamani au ni kubwa sana,yaani kuanzia inch 50 na kuendelea ndio itakuwa shida...
 
Kama unaweza kuibeba projector na kuingia nayo chumbani,kinakushinda nini kuibeba hiyo TV yako wakati TV nyingi za kisasa zinabebeka kirahisi! au kama TV zako ni model za zamani au ni kubwa sana, yaani kuanzia inch 50 na kuendelea...
Nadhani wewe huifahamu Projector. Ungeifahamu usingetoa hoja kama hii.
 
Projector native 4k bei zake ndefu sana halafu haiwezi kuwa full HD na 4k hapohapo. Nyingi bei zake ni milioni 3 kupanda.

Kwa budget zetu za kitanzania HD ama Full HD projector ina make sense zaidi.

Angalia tu eneo lako, umbali wa unapotaka kuiwekea hadi ukuta ulipo, mwanga etc.
So full HD ni nzuri. Well, mtu akitaka Ebay anaweza pata baada ya muda gani? But pia suala la quality ya picha linakuaje hapo?
 
Nini kingine kinahitajika kuipata projector nzuri kwa ajili ya home theatre. Kuangalizia movie/vipindi vya Tv
 
Kama unaweza kuibeba projector na kuingia nayo chumbani,kinakushinda nini kuibeba hiyo TV yako wakati TV nyingi za kisasa zinabebeka kirahisi! au kama TV zako ni model za zamani au ni kubwa sana, yaani kuanzia inch 50 na kuendelea...
Kwa hiyo unataka aipeleke chumbani wamkute chumbani wamtoe roho. Yeye kuiacha sebleni anakuwa na kusudi lake
 
Hii hapa mkuu
Screenshot_20210428-142944_Opera Mini.jpg
 
So full HD ni nzuri. Well, mtu akitaka Ebay anaweza pata baada ya muda gani? But pia suala la quality ya picha linakuaje hapo?
Hivi vitu mkuu vinahitaji uone kwa Macho mwenyewe na mazingira yafanane.

1.Full HD ni nzuri bado kwa mazingira yetu, movies, TV za local, kustream, etc vyote vipo Around HD ama chini ya hapo.

2. Ebay ni Around mwezi mzima, na huyo muuzaji awe analeta huku

3. Kuhusu quality mara nyingi projector unahitaji sehemu yenye giza mwanga mdogo unapata quality nzuri.

Kuna mambo mengine pia kama HDR, 3d, etc yanasaidia kukupa experience nzuri zaidi.
 
4k projector mkuu mbona itakuwa kisu kirefu, ingawaje bado zitakuwa bei chee kulinganisha na TV ya ukubwa wa picha utayoipata toka kwa projector.

Hasara za projector ni kule kufa kwa ile taa yake sababu huwa zinatengenezwa kuhudumu ndani ya masaa kadhaa, hivyo kama ni mtumiaji wa muda mrefu itakulazimu kila baada ya labda mwaka uwe wabadili bulb. Ingawaje wazungu wameweza refusha uhai wa projector kwa kutengeneza zenye kutoa mwanga kwa kutumia LED

Pia itakulazimu uwe na spika za nje, kumbuka TV huja na spika zake ndani "inbuilt" zenye quality nzuri...

Mengineyo wataongezea wadau...
 
Mmh!?,basi kama ndo hvyo,kwahyo niandae tu 1mil au laki 8+ kupata kilicho bora
Sijajua kuhusu masoko used hapa TZ yapoje, lakini ukitaka mpya ndio, around 1m ndio unapata nzuri yenye basic features za ukweli.
 
Projector ni bei sana ndugu, ukiachana na izi projector za laki 3.projector ya EPSON yenye Lumans 3500 ni milioni 2 mkuu.

Lumans 3500 hata mchana unacheki vizuri tu pasipo tabu yoyote ile maana ina mwanga wa kutosha kama vile TV.shida ya Projector uwa lens yake ina muda wa uwezo wake wa kufanya kazi, kwa iyo muda wake ukiisha basi lensi inapoteza nguvu ya kutoa picha nzuri na muda mwingine inazima kabisa mpaka utafute jicho jingine.

Projector yenye lens inayokaa muda mrefu unakuta ina masaa 20000.kwa iyo hayo masaa yakiisha basu jua huna tena projector.

Pia projector ya lumans 3500 ni kama mashine mkuu.unaweza ukashangaa peke yake imekula unit 2.kwa iyo usiingie kichwa kichwa kununua hii mashine, ni bora ununue TV uchomelee nondo
 
Back
Top Bottom