KIFARU
Senior Member
- Apr 6, 2009
- 172
- 15
Maisha ya ndoa jamani yana raha, japo bado sipo huko.Cha muhimu ni kupata yule ambaye Mungu amekuandalia. Utafurahia ndoa yako kama paradiso/mbingu.
Pretty Bravo, Mume/Mke bora utoka kwa Mungu, huku nawe mhusika ukifanya jitihadi kidogo,ni vigumu kumpata mke aliye tulia wakati mwenyewe ujatulia,haiwezekani ukawa mtu wa madisko kisha ukaoa mtu mwenye kushika dini,mimi mwenyewe sijaowa ila maisha ya bila kuoa ni mazuri kwa sababu ndo muda mzuri wa kufahamu tabia za wanawake tofauti,ebu angalia mwendesha baiskeli anayeendesha kupitia njia moja tu kila siku akienda kazini na umfananishe na yule mwenye kubadilisha njia kila aendapo,hakika yule abadilishie njia ndo atakua mtaalam na baiskeli kuliko mwingine,mimi mke nayemtaka kwa sasa najua sitampata kwa sababu vigezo anavyotumia huyo mhusika sinavyo, hivyo sasa hivi wacha nile kwanza lecture ya wanawake na maisha,na kingine muda huu ambao tujaoa tunao si siri ukitaka kupanga mambo yako yanaenda kama unavyotaka labda Mwenyezi Mungu aamue yasitimie,unaweza panga leo najibana nitumie kiasi kidogo cha pesa kinachobaki nitafanyia masuala ya maendeleo, lakini kwenye ndoa kuna majukumu ya lazima huwezi sema ubane pesa wakati kuna tatizo limemtokea mwenzio, nahitimisha kwa kusema single life ni nzuri lakini kuishi na mwanamke kinyumba ni kinyume na maagizo ya Mungu