Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Bora nirudi kwa wazazi wangu wanifunze upya

Story nzuri, inafunzo ndani yake, inaumiza lakini kuna sehemu inatia moyo hasa kwa hiyo commitment binti aliyoionyesha kwa huyo mzee, najaribu kuwaza kama huyu mzee angekua hana ukimwi afu yuko single huyu binti alikua anamfaa sana adse

Anyway that's life
 
Story nzuri, inafunzo ndani yake, inaumiza lakini kuna sehemu inatia moyo hasa kwa hiyo commitment binti aliyoionyesha kwa huyo mzee, najaribu kuwaza kama huyu mzee angekua hana ukimwi afu yuko single huyu binti alikua anamfaa sana adse

Anyway that's life
Mzee amemzingua binti
Amewakilisha wazazi wote wanaoharibu maisha ya watoto wa watu
 
Naomba kuuliza sii kwa ubaya

Hivi mtu km huyu mzee ni mgonjwa au wengine wenye tabia za hivi inakuwa wanafanya makusudi ilihali anajua afya yake ni changamoto dhidi ya mwingine ambaye sio......

Ninunue kile kifaa kabisa kisikosekane kwenye begi huku nje ni kubaya
Vyema kujihami kama unaweza nje kunatisha na hapatabiriki. Na ukweli baadhi hufanya makusudi kwa kudhamiria na wengine ni kutokujali mana si wote wenye kujua afya zao mpaka waskie kuna sehemu waliyopita imelipuka ndo hujihisi na wao tayari.
 
Vyema kujihami kama unaweza nje kunatisha na hapatabiriki. Na ukweli baadhi hufanya makusudi kwa kudhamiria na wengine ni kutokujali mana si wote wenye kujua afya zao mpaka waskie kuna sehemu waliyopita imelipuka ndo hujihisi na wao tayari.
Shukrani boss
 
Pia mzee amepata bahati ya kua na binti anayejitambua
Yule dada muhusika pia alishindwa kumsoma huyo mzee afu ukizingatia ana binti ambaye ni age mate nadhani udhaifu wake ulianza hapo..,..

Kingine hakushtuka kuona ana ukaribu na mwanae licha hawakai nyumba moja!! Akiamini mbaba ata mdekeza kabila gani huyo mchaga nn asiejua kubembeleza au msukuma ni ubabe tuu 😂

Maake huwez Lia vile mtu akuangalie japo wanaume tulio wengi kulia kwako hatuamini ni soln ya changamoto inayokukabili sana sana tutaona utoto km ulivyoeleza kwenye story.......

Mzee mchafu huyo nasubiri kusikia hatma ya bibie kuanza new life!! Without mzee
 
Sawasawa subiri niandike mwendelezo.
Najitahidi kuandika kwa code ili hata Tina akifuma huu uzi asome bila kunijua ila afikirie tu hiki kisa kinafanana na chake😂
Umwambie kisa chake knatoa elimu,especially kwa sisi vijana tunaoanza kuanzisha familia
 
SEHEMU YA 8

Kazi ya Bar sikuwahi kuifikiria katika maisha yangu, ni kawaida kuonekana kama unajiuza na wateja wanakuchukulia poa.

Nimepata kazi sehemu hiihii anayofanyia shoga yangu. Bar hii ni mpya na wateja wengi wanajiweza hata magari yanayopark ni ya kwenda.

Changamoto ya kwanza ni manager, ananiambia kazi nimepata, mshahara ni laki 2 lakini kabla ya kuanza sharti nifanye naye mapenzi.

"Kama ni kufanya naye, tena ni Mara moja tu kwangu sio tatizo. Mimi tayari ni mchafu sina thamani yoyote ile" nilijiambia
Nilikua nimejikatia tamaa kabisa! Kila nikikumbuka nilivyotumika tena kinyume na maumbile nilitamani kujiua.
Nilichotaka ni kukusanya pesa walau ifike millioni 1 ili niweze kwenda kwetu, niende kumuona baba na mama yangu! Imepita miaka mingi sana na Mara zote nikiongea nao huwa wanafuraha wakiamini nimemaliza tu chuo na kupata kazi, bahati iliyoje!

"Shoga! Hata Mimi nililala nae Ndio nikapata hii kazi. Muhimu kumbuka kutumia kondomu, manager amelala na kila mhudumu hapa unadhani atakua nzima?" Rafiki yangu aliniambia nikaishia kumtizama asijue mwili wangu umeshaoza na hivo virusi anavyovihofia.

Nilianza kazi rasmi nikiwa na malengo nikusanye millioni 1 nikawasalimie wazazi.
Kwa siku nilikua nalaza hata elfu 50 kuna wale wa "keep change" wengine wananinunulia bia nazibadilisha pesa.

Nikaanza kupata nuru lakini nilizidi kujichukia!
Nilijichukia sababu nilizidi kubadilisha wanaume.
Mimi nilitaka kumpata mmoja tuwe wote daima lakini wao Mara zote ndio walikua wakinizingua.
......................
Kuna siku nilirudi nyumbani nikamkuta rafiki yangu amekasirika sana na hapo tulikua tushakaa kama miezi miwili tukichangia chumba.

Nilishtuka kuona kopo langu la dawa likiwa kitandani.
BARMAID: Naona ulitaka kuniua, kwanini siku zote hukuniambia kuhusu hali yako? Mambo mangapi tunaongea?

TINA: Sikuona umuhimu wa kusema hata hivyo ningekuambukizaje kwanza? Kwani mtu ukiathirika unatakiwa utangaze?

BARMAID: Wewe sio rafiki wa kweli! Ndio maana hata huyo mzeee alikufanyia mambo ya ajabu! Unabakisha maji, soda Mimi nakunywa kwanini usingekua unakataa? Kiwembe, nailcutter tunashare mpaka nguo. Naona ulidhamiria kuniambukiza.

Alivyomaliza kuongea akaondoka, nilijisikia vibaya nikaanza kulia. Sikumwambia sababu nilidhani ataninyanyapaa.

Nilikua najitahidi kujificha asijue hali yangu. Kubwa zaidi ananikumbushia mambo ya mzee ambayo yanazidi kuniumiza.

Niliyemtegemea anayenionyesha upendo na yeye amenikasirikia. Sikuombea kupata huu ugonjwa, imetokea kwa bahati mbaya tu nikaamua nijiue kwa kunywa panadol.

Nikachukua panadol kama 10 nikanywa nikawa nasubiri nife lakini muda ulizidi kwenda bila kusikia dalili zozote.
 
Back
Top Bottom