SEHEMU YA 8
Kazi ya Bar sikuwahi kuifikiria katika maisha yangu, ni kawaida kuonekana kama unajiuza na wateja wanakuchukulia poa.
Nimepata kazi sehemu hiihii anayofanyia shoga yangu. Bar hii ni mpya na wateja wengi wanajiweza hata magari yanayopark ni ya kwenda.
Changamoto ya kwanza ni manager, ananiambia kazi nimepata, mshahara ni laki 2 lakini kabla ya kuanza sharti nifanye naye mapenzi.
"Kama ni kufanya naye, tena ni Mara moja tu kwangu sio tatizo. Mimi tayari ni mchafu sina thamani yoyote ile" nilijiambia
Nilikua nimejikatia tamaa kabisa! Kila nikikumbuka nilivyotumika tena kinyume na maumbile nilitamani kujiua.
Nilichotaka ni kukusanya pesa walau ifike millioni 1 ili niweze kwenda kwetu, niende kumuona baba na mama yangu! Imepita miaka mingi sana na Mara zote nikiongea nao huwa wanafuraha wakiamini nimemaliza tu chuo na kupata kazi, bahati iliyoje!
"Shoga! Hata Mimi nililala nae Ndio nikapata hii kazi. Muhimu kumbuka kutumia kondomu, manager amelala na kila mhudumu hapa unadhani atakua nzima?" Rafiki yangu aliniambia nikaishia kumtizama asijue mwili wangu umeshaoza na hivo virusi anavyovihofia.
Nilianza kazi rasmi nikiwa na malengo nikusanye millioni 1 nikawasalimie wazazi.
Kwa siku nilikua nalaza hata elfu 50 kuna wale wa "keep change" wengine wananinunulia bia nazibadilisha pesa.
Nikaanza kupata nuru lakini nilizidi kujichukia!
Nilijichukia sababu nilizidi kubadilisha wanaume.
Mimi nilitaka kumpata mmoja tuwe wote daima lakini wao Mara zote ndio walikua wakinizingua.
......................
Kuna siku nilirudi nyumbani nikamkuta rafiki yangu amekasirika sana na hapo tulikua tushakaa kama miezi miwili tukichangia chumba.
Nilishtuka kuona kopo langu la dawa likiwa kitandani.
BARMAID: Naona ulitaka kuniua, kwanini siku zote hukuniambia kuhusu hali yako? Mambo mangapi tunaongea?
TINA: Sikuona umuhimu wa kusema hata hivyo ningekuambukizaje kwanza? Kwani mtu ukiathirika unatakiwa utangaze?
BARMAID: Wewe sio rafiki wa kweli! Ndio maana hata huyo mzeee alikufanyia mambo ya ajabu! Unabakisha maji, soda Mimi nakunywa kwanini usingekua unakataa? Kiwembe, nailcutter tunashare mpaka nguo. Naona ulidhamiria kuniambukiza.
Alivyomaliza kuongea akaondoka, nilijisikia vibaya nikaanza kulia. Sikumwambia sababu nilidhani ataninyanyapaa.
Nilikua najitahidi kujificha asijue hali yangu. Kubwa zaidi ananikumbushia mambo ya mzee ambayo yanazidi kuniumiza.
Niliyemtegemea anayenionyesha upendo na yeye amenikasirikia. Sikuombea kupata huu ugonjwa, imetokea kwa bahati mbaya tu nikaamua nijiue kwa kunywa panadol.
Nikachukua panadol kama 10 nikanywa nikawa nasubiri nife lakini muda ulizidi kwenda bila kusikia dalili zozote.