BORA UBANWE NA HAJA NDOGO/KUBWA SAFARI NDEFU?

BORA UBANWE NA HAJA NDOGO/KUBWA SAFARI NDEFU?

Tatizo lenu mnafakamia mavitu hovyohovyo njiani humo mtaachaje kuhara kabla hamjafika muendapo?? Haiwezekani wew Mahindi, Mihogo, viazi, magimbi, sambusa, wali, kuku, korosho, zabibu, kababu, tende, biscuti, soda vyote vyako..!! Yani kwamba ilo tumbo limegeuka dust bin ?? Utahara tu na mi nasema Muhare
 
Mimi nilibanwa sana na nilipomwendea Konda na kumwomba asimame ili nikojoe akakataa na nilichokifanya kwakuwa mshipa wangu wa aibu ulishakatwa Kitambo na Sister Magreth wa Wodi ya Uzazi Aga Khan Hospital miongo mitatu iliyopita nilichokifanya na kulichomoa tu Libolo langu mubashara na kumkojolea kidogo katika Suruali yake ndipo Dereva nae akashtuka na kusimamisha ghafla Basi Mwanamume nikashuka haraka kukojoa huku Abiria wengine nao wakishuka kwa nguvu na tuliporudi ndani ya Basi wakati likiwa njiani Yule Kondakta akawa anakuja Kwangu taratibu nadhani kulianzisha ndipo nami nikamwoshesha kuwa kuzaliwa tu Dar es Salaam tayari Wewe ni Mjanja ambapo nakumbuka wakati akija usawa wangu nilichomoa Album yangu ambayo ilikuwa ina Picha kadhaa za Kaka yangu ambaye ni Mjeda hivyo nikawa naziangalia hasa zile Picha zake za Mazoezi yao ya hatari huko Kambini na Jamaa alipokaribia pale Kwangu na kuziona tu zile Picha za Kijeda nakumbuka neno moja tu aliloniambia kuwa " Kaka umemaliza Kozi nini? " Nami kwa kutaka kumtisha zaidi nikamwambia nimemaliza lakini sasa naenda Arusha kumalizia Kipengele cha mwisho ili niwe full Commando akanywea / akaufyata na nakumbuka hata tulipofika tu Mombo alininunulia Msosi na Basi lilipofika Arusha alinikodia Tax ikanipeleka nilipokuwa naenda. Mikwara inasaidia sana jamani vinginevyo nisingejiongeza siku zile hakyanani ningepewa nakoz / ngumi za kutosha na yule Kondakta.

Umetunga?
 
Unazungumzia usafiri gani? manake kwenye usafiri nnaoupenda kote nakutana na vyoo, kuanzia boat/meli, ndege, treni.
Samahani kama sikueleweka vizuri, namaanisha hizi safari zenye highway barabarani pamoja na makondakta....Nazungumzia safari za kwenye mabasi.
 
Bora mkojo utaubana.. inafika mahali unashikwa na ganzi ..hupati vile vimaumivu vya kubana mkojo.

Lakin sasa ikushike haja kubwa.. tena uharo... mbona utaelewa... ile hata lisaa humalizi maana pressure yake huwa inatoka bila hiari yako.. unakuta tu kitu kimeshatoka..
 
Nimesafiri safari nyingi sana na nimeshudia visa vya watu kupata wakati mgumu pale wanapobanwa na haja kubwa na ndogo katika safari, Mbaya zaidi mkiwa high way chance ya kupewa ruhusa kwenda kuchimba dawa ni ndogo sana.

Binafsi yamewahi kunikuta...Nilibanwa na haja ndogo basi likiwa kwenye highway, Nilijaribu sana kunegotiate na konda lakini haaikuwezekana maana ilikuwa ni usiku na basi ilibidi liwahi kufika, Nilienda nyuma ambako hakuna watu ili nijaribu kutolea haja kwenye chupa na sikufanikiwa kwa asilimia 100...Ndio ilikuwa siku niliyojifunza kwamba kunywa majia mengi kwenye safari ni sawa na kumtukana mamba kabla safari ya kuvuka mto haijaanza, Thats part of my experience na wewe unaweza kutupatia yako
Nilishuhudia Baba mtu mzima alijipupulia tukiwa safarini, abiria wakachachamaa gari ikasimama akashuka , na mbaya zaidi alishuka kituo ambacho sio chake hadi huruma yaani
 
Back
Top Bottom