Bora uchelewe kuoa au kuolewa ili ukutane na yule mtakaependana kutoka moyoni

Bora uchelewe kuoa au kuolewa ili ukutane na yule mtakaependana kutoka moyoni

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Ndoa nyingi siku hizi zimekuwa zikivunjika mapema sana yaani watu wanaowana baada ya miaka miwili tu ndoa inavunjika na muda mwingine unakuta harusi pamoja na maandalizi mengine yalikuwa ni ya gharama kubwa saana.

Tatizo kubwa nililokuja kuliona asilimia kubwa ya waolewaji wengi wanaolewa na wanaume wasiopenda yaani unakuta mtu anaulazimisha moyo kuishi na mtu na hii ni kwa sababu ya dhiki na maisha magumu kwahiyo anaona bora ajikabidhi kwa mwanaume.

Au wakati mwingine unakuta mwanamke anamsubili anaempenda lakini hatokei...na hapa ndio utakuta anakubali kuishi na mtu asiempenda ili tu na yeye aonekane yuko ndani ya ndoa au ana mume, mahusiano ya aina hii kudumu ni ngumu sana wakuu.
 
hii ni kwa sababu ya dhiki na maisha magumu kwahiyo anaona bora ajikabidhi kwa mwanaume
Wanawakomoa ma-ex hio ndio fashion ya siku hizi mkuu, wanataka ma-ex waumie wanaposikia anaolewa aliona cha nini wenzie wamakiloweka na maji
 
Ndoa nyingi siku hizi zimekuwa zikivunjika mapema sana yaani watu wanaowana baada ya miaka miwili tu ndoa inavunjika na muda mwingine unakuta harusi pamoja na maandalizi mengine yalikuwa ni ya gharama kubwa saana. Tatizo kubwa nililokuja kuliona asilimia kubwa ya waolewaji wengi wanaolewa na wanaume wasiopenda yaani unakuta mtu anaulazimisha moyo kuishi na mtu na hii ni kwa sababu ya dhiki na maisha magumu kwahiyo anaona bora ajikabidhi kwa mwanaume au wakati mwingine unakuta mwanamke anamsubili anaempenda lakini hatokei...na hapa ndio utakuta anakubali kuishi na mtu asiempenda ili tu na yeye aonekane yuko ndani ya ndoa au ana mume, mahusiano ya aina hii kudumu ni ngumu sana wakuu.
Sasa wafanyaje...unataka waendelee na selfie wakati wanamsubiria huyo watakaye mpenda?
 
Mie nina zombie wangu namsubiria tuoane kwenye our late 40s sina papara..

Popote ulipo Sophy one love.

Antonnia shahidi.
Ndio ndioooo shemelaaaa.. Nipe mrejesho kwanzaa mambo yanaendaje !! Mtoto mkareee sana yule katuliaa plus utaenjoy madikodikoo
 
Naona jamii zimevurugika tu.

Hao bibi na babu zetu waliooana mapema na wakadumu kwenye ndoa zao walifanyaje?
 
Back
Top Bottom