Pre GE2025 Bora Uenyekiti wa Mbowe, Lissu bado hajajua watanzania wanataka nini. Mpango wake wa kustopisha Uchaguzi unaenda kuangukia pua!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

..nadhani tuilaumu CCM ambayo inakwamisha mabadiliko.

..haiwezekani CCM iendelee kupiga na kuua watu wakati wa uchaguzi wakati uwezo wa kushinda kihalali wanao.

..sasa hivi CCM wanapokea 3.2 BILLION kila mwezi kama ruzuku.

..wafanyabiashara, wasanii, viongozi wa dini, vyombo vya habari, mahakama, polisi, wote wanaunga mkono CCM, lakini bado wanataka kutumia mabavu.

..Tuwahimize CCM waunde Tume Huru, na uchaguzi ufanyike bila kumwaga damu ya Mtanganyika, au Mzanzibari.
 
Kama anategemea tu maandamano abadilishe plan haraka sana.

Asitegemee watanzania ambao walichagua monopartism over multipartism wakai-pressure CCM kubadilisha sheria kandamizi za Uchaguzi
Swadakta....

Ameshashindwa ,mwamba ni MKAIDI....familia yao ina historia hiyo.....its true something of that sort runs deeply in their genome.....
 

CCM ina madhaifu yake lakini bado watanzania hawajaichoka to the point ya kuandamana ndo maana kila maandamano wanayoita CHADEMA wanafeli.

Kama CHADEMA wanataka mabadiliko wasiwategemee watanzania.

Waangalie alternatives nyingi.
 
Wewe uliona picha mkuu?
Sikuona ndio maana nimeuliza. Tumwamini nani asee, nani anasema ukweli?

Ninavyoeleweshwa ni kwamba vitu kama hivi havitokei nchi za magharibi. Yani huezi sikia mtu au watu wametoweka/kutekwa tu bila ya kuwa na Wananchi makini wakutoa shuruti. Kupiga picha, video n.k Kwamba hata wakenya ni makini sana.

☝️Ila data zao zinakinzana na mtazamo huo juu

###
tukirudi kwenye mada, sidhani kama Watanzania wenzangu ni waoga, mi nadhani Watanzania ni makini.
 

Nakubaliana ila napata kihali kwenye MBINU zinazotumika. .

Hakuna kitu CHADEMA na Lissu wata-achieve wakitegemea watanzania kuandamana. It has been proven once and again kwamba maanadamano kwenye nchi hii haya-work.

Mifano ipo ya kutosha.

Nimependa aya ya mwisho umesema TUWAHIMIZE hao CCM.

Tunawahimiza kwa mbinu gani hapo ndio MZIKI uliopo!
 
Waangalie alternatives nyingi.
Kama zipi Mkuu. Sie tulio ndani tunachukua ushauri wowote na kuzifanyia kazi.

What other alternatives kama CCM bado ""haijatubana" according to you tunaeza tumia?
 

Na hata mimi sidhani watanzania ni waoga.

Ni kwamba tu CCM has not done enough evil to the point ya kuwafanya watu waandamane.

Ndo maana mwanzo nikagusia suala la timing.

Watanzania hawana tofauti na wachina
 

..nguvu tunazoelekeza kuwakatisha tamaa wapinzani tuzielekeze kuwahimiza CCM walete mabadiliko ya kweli.

..Ni jukumu letu sisi ambao tuna uelewa kupaza sauti kwa namna mbalimbali kwa ajili ya Tanzania bora zaidi.

..Sio sawasawa watu wanatekwa, wanapotezwa, wanauwawa, halafu tunawabeza wale wanaopinga vitendo hivyo, badala ya kuwakemea wanaofanya unyama huo.
 
Kama zipi Mkuu. Sie tulio ndani tunachukua ushauri wowote na kuzifanyia kazi.

What other alternatives kama CCM bado ""haijatubana" according to you tunaeza tumia?

Nimetaja hapo mkuu kwenye bandiko langu

Lissu asitegemee wananchi maana hata mfumo wa multipartism Tanzania HAUKULETWA na wananchi.

Uliletwa na elites na foreigners

Kwa hiyo ni either Lissu arudi kwa elites wa CCM wakazungumze au aende foreigners waliotuletea mfumo waipe pressure CCM
 
Mungu akubariki sana gentleman kusema ukweli 🐒
 
Na hata mimi sidhani watanzania ni waoga.

Ni kwamba tu CCM has not done enough evil to the point ya kuwafanya watu waandamane.

Ndo maana mwanzo nikagusia suala la timing.

Watanzania hawana tofauti na wachina

..tukiacha mambo yaharibike mpaka watu waingie mitaani tutakuwa tumeitendea haki nchi yetu?
 



Mkuu labda hujaelewa hoja yangu.

Siko hapa kuwabeza CHADEMA na ndio maana kwenye bandiko langu ukiachana na kusema approach ya Lissu sio nzuri pia nimetoa na practical SOLUTIONS

Hivi ni mara ngapi CHADEMA wameitisha maandamano watu wanagoma kwenda?

Kwa miaka ya nyuma enzi za M4C CHADEMA walikuwa na nguvu kuliko now, walikuwa wanaitisha maandamano wamachama wao wanapigwa, wanarudi nyumbani.

Ni sheria gani ambayo CCM walishaibadilisha kwenye nchi hii kwa sabanu ya maandamano ya CHADEMA?
 
Na hata mimi sidhani watanzania ni waoga.

Ni kwamba tu CCM has not done enough evil to the point ya kuwafanya watu waandamane.

Ndo maana mwanzo nikagusia suala la

timing.

Watanzania hawana tofauti na wachina
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kwa mtazamo huo basi napinga;Si warefu bana


ila ww mzee naona kama unakwepa goli kwa kuhamisha magoli.

Ni alternative gani ambayo Mh. LISSU anaeza tumia na Wananchi wakamkubali?


Tunajua, ni chaguo la mungu, tunajua ana akili kubwa sana, tunajua ni mtetezi wa haki, tunajua ni mchapa kazi, kimsingi, ana mapungufu machache ukilinganisha na Mh.Mbowe na wengine wanaolinganishwa nae.

Mh. LISSU afanye nn kama hamna Erections za Watu?
 

..uongozi mpya wa Chadema haujatimiza hata mwezi mmoja, tayari unatoa hukumu kwamba uongozi uliopita ulikuwa na afadhali.

..ndio maana nasisitiza kwamba tujiepushe na kauli za kuwakatisha tamaa watetezi wa haki hapa Tanzania.

..tuachane na kauli zinawatia nguvu watesi wetu, na kuwavunja moyo watetezi wetu.
 
I hope atafanya hivyo. CCM wanawaogopa wazungu kuliko watanzania

In fact ni wazungu walioshinikiza mfumo wa multipartism kwenye nchi hii.

Watanzania walikuwa hawautaki
Ilikuwa enzi hizo,sio leo.Ushawishi wa demokrasia ya Magharibi kwa nchi za Africa unazidi kushuka,Africa inategemea sana China.
Uchumi wa China na nguvu yake ya kijeshi ni kubwa sana.
Marekani na nchi za Magharibi wana mikopo mikubwa kutoka China ya utawala wa kikominist.
Vita vya Urusi na Ukraine vimeigawa Ulaya na Marekani chini ya Trump.Wazungu wako busy kutatua matatizo yao kwanza.Hawana muda wa Africa, angalia machafuko ya Sudan,DRC n.k
 
Lissu hajui Mtanzania wa leo anahitaji nini?, mtanzania huyu sio yule wa 1990-2020, mtanzania huyu ni mwingine kabisa, mosi, huwezi kumswaga kwa mambo ya kipuuzi, pili anapima hoja, anapima na hali za ulimwenguni unavyokwenda, anaangalia Congo, Msumbiji, anafanya kulinganisha na upuuzi wa mwanasiasa, anashtuka, mwishowe anagundua kumbe mwanasiasa yeye yupo kazini kwake, na anavyo tutia ghadhabu na kutupandisha mori na kututia chaka bovu / mkenge ndio yeye mapato yake yanaongezeka.
Siasa ni ujinga fulani ukishindwa kuustukia utakupotezea mda mwingi sana, wenye uelewa wanagombea nafasi ndani ya chama ili walipwe hakuna kazi ya hasara hapa duniani na wakati ni fedha na ustawi wa kimaendeleo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…