Hata CHADEMA na watu ambao hawana vyama wote wakisema hawaendi kupiga kura mamilioni ya wanachama wa CCM wataenda kupiga kura na uchaguzi UTAFANYIKA kwa sababu CCM bado wana millions of wanachama.
Kwa hiyo haitabadilisha kitu
Hivi unadhania watu kama kina Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah wako wangapi kwenye nchi hii?
..nadhani tuilaumu CCM ambayo inakwamisha mabadiliko.
..haiwezekani CCM iendelee kupiga na kuua watu wakati wa uchaguzi wakati uwezo wa kushinda kihalali wanao.
..sasa hivi CCM wanapokea 3.2 BILLION kila mwezi kama ruzuku.
..wafanyabiashara, wasanii, viongozi wa dini, vyombo vya habari, mahakama, polisi, wote wanaunga mkono CCM, lakini bado wanataka kutumia mabavu.
..Tuwahimize CCM waunde Tume Huru, na uchaguzi ufanyike bila kumwaga damu ya Mtanganyika, au Mzanzibari.