Hivi hao form six wenye akili wanapatikana vyuo gani huko nije kufanya utalii wa ndani?
Maana kwa uzoefu nilioupata katika utafiti wangu usio rasmi, nimetoka chuo fulani hivi karibuni, ni kati ya vyuo vikubwa kabisa nchi hii na kinasifika kwa kutoa products za maana, ila products (in the making) zenyewe nilizozishuhudia hadi najionea aibu mwenyewe.
Si diploma si form six tabu tupu, watoto wa 2000 kazi sana, yaani vichwa vipo empty hadi unashangaa. Ukiwakuta wamekaa kwenye vimbweta wana arguments kama za mleta mada, wakisimuliana jinsi walivyopata div I huku wakikaririshana notes neno kwa neno.
Kuna wachache sana wenye uwezo binafsi wanafanya vizuri, na huwa haijalishi katokea diploma au form six.
Binafsi naamini elimu ilikuwa zamani, ila ya sasa hata division one hazina chochote kichwani. Unabaki ukijiuliza kama hizi ndo div I za Leo, je III na IV zitakuwa na hali gani?! Hata wakufunzi wanajua na wanatunga mitihani rahisi ili kuendana na kizazi, la sivyo supplementary, carry-overs na discontinuation zitamaliza darasa. Hata past papers za miaka ya nyuma inaonesha tofauti kubwa ukilinganisha na ya sasa. Mitihani ya zamani iliwataka watahiniwa kufikiri, ya leo inawataka kukariri. Wakifanikiwa kukariri wakafaulu, wakaongezewa na marks kadhaa wakapata A au B+ wanasahau kuwa walifanyiwa boosting, wanaanza kutambia uwezo wa akili na muda huo wameshasahau kila walichokisoma kabla ya mtihani!
Kwa ufupi elimu yetu inahitaji mabadiliko makubwa sana, maana kwa sasa ni bora liende tu kukuza mtaji wa ccm wa wajinga waliosoma wa kujazana uvccm na uchawani.