Bosi wa bahari barbershop nakufikishia haya malalamiko

Status
Not open for further replies.
Kiukweli nimeumia. Ukiona mwanaume anakuomba hela mpe bro hata kama huna tumia tu diplomasia kumjibu mzee. Hukuwa na haja kutangaza shida ya mtu hadharan. Nakumbuka cku moja nimetoka China pale airport nikiwa naelekea kwenye gar tulikuwa kama watatu alikuja polis mtu mzima kidogo. Akatuomba hela. Na ninakumbuka maneno yake mpaka leo. Wadogo zangu polen na safari naomba kama kuna hela yoyote imebaki mnipe kuna wadogo zenu wamerudishwa shule hapa nilipo cna kitu na nimewaahid jion nitawaletea.
Itoshe tu kusema nilimvuta pemben akanieleza shida zake mpaka nikatoa machozi. Wanaume tunapitia moto ni Mungu anajua. Niliomba majina ya watoto wake na shule wanazosoma nilimlipia ada zote nikamtumia results slip . Kama yupo humu atanikumbuka. Ila Mungu ninani hata asinikumbuke mzigo ulivyotoka mzambia aliuchukua wote conteiner zima akalipia benki. Na ndio chanzo cha Mimi kuamin katika kutoa bila kunung'unika.
 
Binafsi Niko direct, kama ninayo mfukoni nakupa moja Kwa moja wala sipepesi mara mbili hasa akiwa mwanaume coz wanaume wana hali mbaya sana kipindi hichi, kama Sina tutatumia diplomasia tutaelewana then Kila mmoja anapita njia yake, kama huna tena aliyekuomba ni mwanaume mwenzako ni jambo dogo tu la kuongea sekunde kadhaa kuwa huna, Yan ile lugha ya kiume na ya kishkaji zaidi...ILA ISIWE MAZOEA KWANI HUJENGA TABIA.
 
Hatufanani mkuu.
Vinyozi wana hali ngumu, ukimpa 2k tu anafurahi, kulalamikia kitu cha hiyari kwangu naona si sahihi.

Lakini pia sishangai, kuna watu huwa hawatokwi hata mia yani hii hata kwa wazungu ipo, wapo wazungu bahili mnoo hata tips hawatoi
Kuna watu wabahili htree.... Na sipendi circle yangu iwe na hao watu.... Maake watakufanya km kitega uchumii,
 
Saluni hakuna akauntanti kuna keshia tu
 
Mimi siku ikipita bila kutoa tip sijisiki vizuri...hasa kwa walinzi wa magetini, vijana wachakarikaji barabarani, wasafisha vyoo kwenye mabaa,waiters ,wamama wanauza matunda etc barabarani. Etc..tuwe na moyo wa kutoa tip ni kitendo cha baraka zile shukrani zao ni baraka kubwa sana.
 
Kutoa ni Moyo, wengine wakitoa mpaka kwa wanawake tu ili wawaombe mzigo baadaye, na sio Moyo wakusaidia tu.
 
Ningekua Mimi ndio wewe ningeitaja hii Bahari iko Mkoa, Wilaya, Kata, mtaa, kitongoji gani
 
Kwa wanaume wenzio kama una uwezo we watoe tu, ila Kuna yale magume gume yanalala na leo huyu kesho yule, kwenye room ya massage yanafanya matusi humo humo kwa siku mala kadhaa, hayo usiyape hata mia
 
Tip muhimu kama mtu kakuhudumia vizur,iwe saloon,kwenye mgahawa nk hawa ndugu zetu wape tu Mungu atakuongezea 🙂
 
Bei ya kunyoa ni elfu kumi nalipia pale kwa accountant naondoka naenda kwenye gari langu nataka kuondoka kinyozi ananifata kwenye gari ananiomba Tena hela, yaani nilipe Mara mbili kwel hii sio sawa mzee wanatufukuza wateja.
Jaribu siku moja usiende na gari uone kama watakufuata
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…