Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Katika hili, BOT ni kama wamelala, tena usingizi wa pono, kwani bado ziko taasisi za kifedha zinazokaa na kadi za Benki za wateja wanaoenda kuomba mikopo kama moja la shariti la kupewa mikopo wakiamini kukaa na kadi ya mteja ndio security ya fedha zao.
Ukweli ni kwamba, kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, wakopeshaji kukaa na kadi za wateja wao hakutoi tena security ya fedha wanazokopesha kwani siku hizi mtu unaweza kuhamisha fedha kwa kutumia simu ya mkononi mara tu mshahara unapoingia (unapopata sms).
Kwahiyo,wakopeshaji hawa kukaa na kadi ni swala tu la mazoea kwani kama mteja sio muaminifu, anaweza tu kuhamisha fedha kwa kutumia simu yake na kadi isiwe na msaada wowote na zaidi hawezi kwenda kushitaki popote kwani mwenyewe anavunja sheria kukaa na kadi ya Benki ya mteja.
Kitendo cha taasisi hizi ndogo ndogo za kifedha kukaa na kadi za wateja kinaleta usumbufu kwa wateja wao pale wanapokuwa wamesafiri na mishahara ikatoka wakiwa safarini either kikazi, likizo au kuhudhuria misiba na hata mtu anapohitaji huduma kama bank statement n.k.
Hivyo,tunaishauri Benki Kuu kuweka msisitizo wa katazo hili na zaidi waendeshe msako wa kushitukiza tarehe za mwisho wa mwezi mishahara inapotoka ili kuwabaini wale wanaondelea kukiuka sheria.
Pia, kukaa na kadi kunanufaisha mawakala wa mabenki wanaotumia mashine zao kutoa fedha kutoka kwenye akaunti za wateja na kuumiza wateja(wakopaji) kwani makato kwenye hizi mashine ni makubwa tofauti na makato ya kwenye ATM ambayo ni nafuu. Katika hili, naamini mabenki wana nafasi nzuri ya kugundua mawakala wanaoshirikiana na wakopeshaji kutoa fedha kupitia mashine hizi kwa kuangalia transactions zinazofanyika kwa wingi kila mishahara inapotoka.
BoT fuatilieni hali hii na muikomeshe kwani haipendezi na pia si salama kwa watu kutoa namba zao za siri kwa mtu ambae kadi ya benki sio yake.
Watumishi wa nchi hii wanapita kipindi kigumu sana awamu hii na kulazimika kuishi kwa madeni huku kadi zao za benki zikimilikiwa na wakopeshaji wakati sheria hairuhusu.