BoT fanyeni msako wa kushitukiza, bado ziko taasisi za kifedha zinazokaa na kadi za benki za wateja wao

Tatizo BOT wamelala.
Unafikiri wamelala basi? Kuna waliokwisha wajibishwa tayari ili wawe mfano kwa wenzao lakini hao wenzao wenyewe hawaelewi wanaendelea tuu kuhujumu uchumi

Yakiwakuta wanaanza kulialia

Kukopesha kwa aina yoyote bila kuwa na kibali cha BOT na kufuata taratibu zake ni kosa la uhujumu uchumi
Hakuna utaratibu inamruhusu mkopeshaji kuhold kadi ya bank ya mkopaji
 
We acha kutetea upuuzi. Mishahara duni ni chanzo kikubwa cha haya yote. Jiulize ni kwanini watumishi wa hali ya chini tu ndio wanaocha kadi na si vibosile au wale wenye marupurupu mengi?

Hii mishahara sio tu haitoshi, bali haikidhi hata maihitaji ya msingi na ndio maana watu wanaacha Utumishi wa umma na kukimbilia kwenye siasa au hata kwenda private.

Mishahara serikalini ni duni tangu siku nyingi ila awamu hii imeifanya iwe duni mara mbili na hivyo kuongeza tatizo ambalo teyari lilikuwepo badala ya kulipunguza.

Msitetee huu unyonyaji kwa kisingizio mishahara huwa haitoshi.
Unamaanisha nini unaposema niwatumishi wa hali ya chini peke yao ndio wanaokopa kwenye vibanda umiza?? Hivi vibanda umiza wanakopa watumishi wa kila aina hadi wakulugenzi madaktari wasomi wakubwa hadi na wale wale walioko makao makuuu watumishi wa office za kimataifa wote niwateja wao hadi mameneja wabenki nao niwateja watiiifuuu kwenye hivyovibanda umiza. Kwahiyo kinachowapeleka huko siokwamba nimishahara duni.

Suala la kukopa ni la mtu binafsi na maisha yake. Kunawatu hawana hatahuo mshahara duni lakini siowateja wa hivyovibanda umizaaa. Kinachotugarimu wengi nikutaka kuishi maisha yaliyo inje na pato letu hasa tukitakakushindana na matajiri wakubwa.

Mfano, unakuta mtu anamshahara wa laki tano kwa mwezi halafu anataka naye akasomeshe shule ya private ya kulipa ada kwa mwaka milioni 4, kisa tuu anataka kushindana na mfanyabiashara mkubwa maalufu Tanzania, sasa huyu mfanyakazi ataacha kujipeleka kwa vibanda umiza ili akope kukidhi hayo maisha aliyojitengezea bila kuwa na sababu ya msingi?? Tuache tamaa tuendane na uhalisia wa kipatochetu.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Unafikiri wamelala basi? Kuna waliokwisha wajibishwa tayari ili wawe mfano kwa wenzao lakini hao wenzao wenyewe hawaelewi wanaendelea tuu kuhujumu uchumi

Yakiwakuta wanaanza kulialia

Kukopesha kwa aina yoyote bila kuwa na kibali cha BOT na kufuata taratibu zake ni kosa la uhujumu uchumi
Hakuna utaratibu inamruhusu mkopeshaji kuhold kadi ya bank ya mkopaji
Hao BOT mnawaonea, ni sisi wenyewe raia tunaojipeleka kukopa kwenye vibanda umiza nyakati za asubuhi na usiku na kujichomeka kwa kila sheriti utakalopewaa. Fikilia kwa mfano, unakutana na mtu anakubembeleza tena kwa machozi akitaka umpe laki moja mwisho wa mwezi akuleteee laki moja na nusu kisa tuu akanywe mbege. Unadhani mkopeshaji ataacha kumpa?? Pia hata raia wenyewe hawako tayari kulipotisha tukio.
 
Kwa mfano, Kwenye ATM za benki ya NMB Wilayani Sikonge ,Kuna vijaaa wakurya ndiyo mawakala wa kukopesa,huwa wanashinda pale Benki wakiwa na mamia ya Kadi za wadaiwa.

Hivyo kila anayedaiwa akifika ATM wale vijana wanatoa pesa zao Kisha mdaiwa wanampa pesa kiasi silizosalia na wanabaki na Kadi,Tena mbele ya viongozi wa Benki na asikari walinzi.
Hata huku wapo.
 
Nilishaliona pia hilo pale ATM za NMB Korogwe Kuna wakuria ofisi zao zipo jirani na Ofisi za Tigo Korogwe, nap ni hivyo hivyo .cha ajabu mtu ukikopa riba yao ni 50% huu wizi wa mchana
 
Hao BOT mnawaonea, ni sisi wenyewe raia tunaojipeleka kukopa kwenye vibanda umiza nyakati za asubuhi na usiku na kujichomeka kwa kila sheriti utakalopewaa. Fikilia kwa mfano, unakutana na mtu anakubembeleza tena kwa machozi akitaka umpe laki moja mwisho wa mwezi akuleteee laki moja na nusu kisa tuu akanywe mbege. Unadhani mkopeshaji ataacha kumpa?? Pia hata raia wenyewe hawako tayari kulipotisha tukio.
Huyo anayekubembeleza anafanya hivyo sababu ya uhitaji, na wakati huo yuko desperate anaweza fanya lolote apate pesa ilaila hiyo haikuruhusu wewe kuvunja sheria kwa kuchukua kadi yake ya bank.
Achana na kuchukua kadi za watu maana kosa likidhihirika kwako adhabu yake ni kalii
 
We we unadhani bilakuelimishwa kwa huyo anayetafuta mkopo unadhani mpokeaji ataacha kuzichukua hizo kadi za benkii?? Halafu ifahamike kwamba siokala anayekopa anamaisha magumu, wengine walio wengi ni starehe zao tuuu. Wapo wanaonadi maashamba na nyumba. Na hiii imetokana kwamba sikuizi wizi wa sasa nimkopo, ukimkopesha mtu fedha bila kushika kitu hiyofedha nisawa na kumpa bure. Kwahiyo hizosheria ziende kwa raia wote wenyemawazo ya kukopa na kuacha kadi, na sio kwa mkopeshajii.
 
Kwa mujibu wa regulators kupitia sheria, taratibu na miongozo adhabu kali itatolewa kwa yoyote unayekopesha fedha nje utaratibu sio kwa anayekopa

Usishangae ukijikuta keko kwa ajili ya riba ya elfu30 uliyomtoza mwananchi
 
Nimesoma makala yako. Nimesoma komenti za watu na wengi wanadhani tatizo hili linawakabili zaidi walimu, manesi na watumishi wengine wa kawaida...

Nawahakikishia kuwa HUU SIYO UKWELI. "Mikopo" ni roho tena ya kuzimu ambamo ndani inasukumwa na tamaa, ufahari, sifa (kukwezwa au kujikweza), ulafi, uasherati, ulevi, uzinzi nk

Roho haijamwacha mtu yeyote wa cheo chochote na rika na jinsia yoyote salama..

Wabunge wako kwenye mikopo, mawaziri wako kwenye mikopo, nchi ziko kwenye mikopo nk nk...

Tofauti kubwa ni moja tu. Nayo ni kuwa UMEKOPA WAPI na KWA MASHARTI GANI..

Lakini UKWELI ni kuwa wote wanaogelea kwenye madeni yanayotokana na mikopo...!!

KUHUSU HOJA YAKO HII SPECIFIC, Haya ndiyo maoni yangu:

Kwamba, kuna mambo kadhaa yanayoleta ugumu wa taasisi za serikali kama ulivyosema BoT, polisi, TAKUKURU, TISS nk kudhibiti hili

1. WATU KUPENDA FEDHA KULIKO UTU: Hizi ni nyakati zilizotabiriwa, watu kupenda fedha sana kuliko utu. Siku hizi ni ngumu sana kusaidiana. Kama tupo tunaosaidia bila sharti la kutumia shida ya mtu mwingine kujipatia faida, basi ni wachache sana . Imefika wakati unaenda kwa jamaa, ndugu au rafiki akusaidie pesa una shida anakupa kwa sharti umrejeshee na riba fulani...Kwa hiyo yameruhusiwa yatokee. Ni nyakati za "hapendwi mtu ila pochi tu..."

2. UKOSEFU WA UAMINIFU: Hilo la kwanza linasababishwa na binadamu wa nyakati hizi wanaokopa na wakopeshaji kukosa uaminifu. Wanaokopa ni walafi sana wa fedha. Hii inathibitishwa na kiwango cha riba. Kopa 1,000,000 rudisha 1,400,000 au zaidi kwa mwezi. Riba kati ya 40% na 50%. Hakuna tafsiri nyingine hapa mtu aweza kuitoa isipokuwa huu ni WIZI wa mchana kweupe..

Sasa ili kujihakikishia wanapata chao hiki cha wizi kwa kutumia shida za watu, wanabuni njia kama hii ya kumbana mkopaji awe hana njia ya kukwepa kurejesha fedha yao...

3. MIKATABA YA UKOPESHAJI: Wakopeshaji hawa ni wajanja sana. Haiko kama unavyofikiri. Hakuna kipengere kwenye mkataba kinachosema mteja kaacha Kadi ya bima ya afya au ATM kadi kama dhamana take

Aidha mikataba hiyo haioneshi mteja kakopa shilingi ngapi kwa riba kiasi gani. Kinachosomeka kwenye contract ni mkopaji kakopa Tshs 6,300,000 na atarejesha kwa awamu au miezi 18 ya kila mwezi 350,000/=. Kumbe masikini mkopaji huyu alichochukua mkononi mwake ni 2,000,000 tu...!!!

Kwa hiyo unaweza kuona kuwa, mkataba wa namna hii hata mkienda mahakamani, mkopeshaji atashinda kesi kirahisi tu...

Hata hizo kadi za bima ya afya au za benki (ATM) wanazoacha wakopaji kama dhamana kwa wakopeshaji hawa wa mitaani hutaweza kuwakàmata nazo hata uwavamie usiku wa manane...

Hili linawezekana tu kama mkopaji mwenyewe atatoa ripoti polisi kwamba, bwana fulani ameshikilia kadi yangu ya benki/bima ya afya...

4. SHIDA NA MATATIZO:
Watu wengi huingia kwenye mikopo hatarishi kama hii kwa sbb ya shida. Shida ikimkuta mtu, uvumilivu wa kusubiri huwa haupo na mara zote tunakuwa hatuna choice. Kwamba, popote tunapoweza kupata fedha au tunachokihitaji kwa masharti yoyote tutaingia huko...

5. SI RAHISI KUMSALITI ALIYEKUSAIDIA:
Wakopeshaji hawa wana umuhimu wao. Wanasaidia sana watu. Mokpo yao haina urasimu. Ni pesa za papo kwa papo. Ni tofauti na benki ambapo huchukua kati ya siku 3 hadi wiki 2 kupata fedha...

Tatizo la hawa ndugu zetu ni riba kubwa kwenye mikopo yao kati ya 40% na 50%. Hii siyo haki hata kidogo..

Pamoja na hayo, wanakuwa wamesaidia. Ni ngumu kidogo kumshitaki au kuingia mgogoro na aliyekusaidia hata kama ni kwa masharti dhalili na magumu kidogo...

Kwa hiyo mtu anapoacha kadi ya Benki (ATM) au ya Bima ya Afya ama chochote kinachompa uhakika mkopeshaji kurejeshwa kwa fedha yake, basically inakuwa ni "mutual agreement" kwa mkopaji kukubali mwenyewe kwa hiari...

6. Haya ndiyo maisha in this "UNFAIR WORLD" ya Leo. Wenye kingi wanaendelea kuwa navyo vingi zaidi huku wakiwanyang'anya wasionacho hata kile kidogo walichonacho....

It's quite difficult kwa mamlaka kulidhibiti hili kwa sababu nilizoeleza hapo juu...

SASA TUFANYEJE?

La kufanya ni kuendelea kufundishana na kushauriana. Hili ni tatizo la kiroho lililoko ndani mtu mwenyewe mmoja mmoja. Sheria inaweza kufanya kidogo sana kulidhibiti lakini haiwezi kuliondoa au kulikomesha...

Ushauri wangu mimi ni

A: Watu turudi kule tulikokuwa kwenye UTU, UBINADAMU na UAMINIFU na kuishi KINDUGU..

B: Watu tuishi kwa MIPANGO na BAJETI kulingana na uwezo wa kila mmoja. Tusipende kufanya mambo zaidi ya uwezo tulionao. Kama huna fedha ya kumsomesha mtoto au watoto kwenye shule ya gharama ya Tshs. 3,000,000 au 4,000,000 kwa mwaka wakati kipato chako cha mshahara ni 500,000 kwa mwezi, usimpeleke huko badala yake mpeleke shule za serikali zilizo na gharama nafuu na fuatilia maendeleo yake na kumlea vizuri ktk msingi wa maadili, nakuhakikishia atafanya vizuri tu ktk masomo yake...

C: Tuepuke TAMAA na kutamani UFAHARI na SIFA toka kwa watu. Ishi maisha yako. Usiichi maisha ya mtu mwingine, utaumia bure. Tukipenda haya, utaingia kwenye FEDHEHA na AIBU siku zote. Maana utaishi kwa kuiga maisha ya watu wengine..

D: Tuwe wabunifu kwa kutafuta vyanzo vingine vya kutuingizia mapato nje ya mishahara. Utumishi wa "mshahara" siku zote ni ubunifu wa wenye navyo kuwafanya watumwa wao wale wasiokuwa navyo. Mtego uko hapa. Tulione hili na tusikubali mtego huu kutukamata...

D: Tufanye kazi kwa bidii na maarifa yote. Tusitegemee chanzo kimoja cha kipato yaani mshahara. Tulio kwenye maeneo ya ardhi pana, tusidharau kilimo. Tukienzi na kitatutoa kwenye umasikini na kutupa maisha ya heshima. Utajiri na fedha zote ziko kwenye ardhi na kwenye maji na angani. Tuwekeze huko...

E: ABOVE ALL, siku zote tujifunze kuishi kwa kumtegemea Mungu Baba muumba wetu. Yeye ndiye aliyetuumba. Anajua tunahitaji kula, kunywa, mavazi, nyumba za kuishi, usafiri (Magari au Pikipiki au baiskeli nk). Tufanyeni kazi kwa sababu KAZI NI BARAKA...

KOPA MARA MOJA, KISHA WEKEZA MKOPO HUO UZALISHE. Usiishi maisha ya mikopo miaka yote, NI AIBU na FEDHEHA mno. Wengine familia zimesambaratika kwa sababu ya mikopo...!!
 
Huyu inawezekana anafanya hii biashaara na ndio maana anatumia nguvu nyingi kutetea huu udhalimu.
 
Noted!
 
Katika hili, BOT ni kama wamelala, tena usingizi wa pono, kwani bado ziko taasisi za kifedha zinazokaa na kadi za Benki za wateja wanaoenda kuomba mikopo kama moja la shariti la kupewa mikopo wakiamini kukaa na kadi ya mteja ndio security ya fedha zao.

Ukweli ni kwamba, kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, wakopeshaji kukaa na kadi za wateja wao hakutoi tena security ya fedha wanazokopesha kwani siku hizi mtu unaweza kuhamisha fedha kwa kutumia simu ya mkononi mara tu mshahara unapoingia (unapopata sms).

Kwahiyo,wakopeshaji hawa kukaa na kadi ni swala tu la mazoea kwani kama mteja sio muaminifu, anaweza tu kuhamisha fedha kwa kutumia simu yake na kadi isiwe na msaada wowote na zaidi hawezi kwenda kushitaki popote kwani mwenyewe anavunja sheria kukaa na kadi ya Benki ya mteja.

Kitendo cha taasisi hizi ndogo ndogo za kifedha kukaa na kadi za wateja kinaleta usumbufu kwa wateja wao pale wanapokuwa wamesafiri na mishahara ikatoka wakiwa safarini either kikazi, likizo au kuhudhuria misiba na hata mtu anapohitaji huduma kama bank statement n.k.

Hivyo,tunaishauri Benki Kuu kuweka msisitizo wa katazo hili na zaidi waendeshe msako wa kushitukiza tarehe za mwisho wa mwezi mishahara inapotoka ili kuwabaini wale wanaondelea kukiuka sheria.

Kukaa na kadi kunanufaisha mawakala wa mabenki wanaotumia mashine zao kutoa fedha kutoka kwenye akaunti za wateja na kuumiza wateja(wakopaji) kwani makato kwenye hizi mashine ni makubwa tofauti na makato ya kwenye ATM ambayo ni nafuu. Katika hili, naamini mabenki wana nafasi nzuri ya kugundua mawakala wanaoshirikiana na wakopeshaji kutoa fedha kupitia mashine hizi kwa kuangalia transactions zinazofanyika kwa wingi kila mishahara inapotoka.

BoT fuatilieni hali hii na muikomeshe kwani haipendezi na pia si salama kwa watu kutoa namba zao za siri kwa mtu ambae kadi ya benki sio yake.

Watumishi wa nchi hii wanapita kipindi kigumu sana awamu hii na kulazimika kuishi kwa madeni huku kadi zao za benki zikimilikiwa na wakopeshaji wakati sheria hairuhusu.
KUNA TAASISI MOJA YA KIFEDHA INAPATIKANA HAPA MWENGE KIVULINI.AISEEE HAWA JAMAA WANAWAUMIZA SANA WALIMU WA SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI.MZEE BABA HAWA JAMAA WANAKUPA MKOPO LAKINI SHARTI LAO NI KWAMBA UNAWAPA KADI YA BENKI,UNAWAPA NA PASS WORD ZAKO, WANAKUTOA ADI KWENYE SIMU BANKING YAN ALAFU WANAINGIA WAO KWA PASSWORD ZAO MPYA,I UNAWAPA CODE ZOTE NDIO WANAKUPA MKOPO YANI.

RAIS WANGU MAGUFULI WAFUATILIE HAWA JAMAA WANAITWA MHELE COMMERCIAL AGENCY (MCA) WAPO HAPA MWENGE KIVULINI YANI UKIJARIBU KUFANYA SURPRISE VISIT WALE JAMAA UTAKUTANA NA KADI ZA BENK ZA WATEJA KAMA MIA MBILI NA USHEEE WAMEZIKAMATIA OFISINI KWAO. WANAWAFANYA WALIMU KAMA WATUMWA WAO.WANA DRAW HELA YAO THEN WEWE UAENDA KUCHUA KILICHOSALIA AISEEE HII NCHI HAWA JAMAA WATATUUA

CHONDE CHONDE GAVANA WANGU WA BOT PROF LUOGA VAMIA PALE ATA LEO JIONI I SWEAR WAMEKAMATA KADI ZA BENKI ZA WANANCHI WANYONGE YANI MWANANCHI HANA ACCESS TENA NA MABO YA BENKI MPAKA WAKIMALIZA MAREJESHO YAO NDIO WANAKURUDISHIA KADI NA PASSWORD YAKO BAADA YA WAO KUTOA YA MWANACHI NA KUINGIZA ZA KWAO AISEEE NI HATAREEEEEEEEE.

MIAKA MITANO TENAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
KUNA TAASISI MOJA YA KIFEDHA INAPATIKANA HAPA MWENGE KIVULINI.AISEEE HAWA JAMAA WANAWAUMIZA SANA WALIMU WA SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI.MZEE BABA HAWA JAMAA WANAKUPA MKOPO LAKINI SHARTI LAO NI KWAMBA UNAWAPA KADI YA BENKI,UNAWAPA NA PASS WORD ZAKO, WANAKUTOA ADI KWENYE SIMU BANKING YAN ALAFU WANAINGIA WAO KWA PASSWORD ZAO MPYA,I UNAWAPA CODE ZOTE NDIO WANAKUPA MKOPO YANI.

RAIS WANGU MAGUFULI WAFUATILIE HAWA JAMAA WANAITWA MHELE COMMERCIAL AGENCY (MCA) WAPO HAPA MWENGE KIVULINI YANI UKIJARIBU KUFANYA SURPRISE VISIT WALE JAMAA UTAKUTANA NA KADI ZA BENK ZA WATEJA KAMA MIA MBILI NA USHEEE WAMEZIKAMATIA OFISINI KWAO. WANAWAFANYA WALIMU KAMA WATUMWA WAO.WANA DRAW HELA YAO THEN WEWE UAENDA KUCHUA KILICHOSALIA AISEEE HII NCHI HAWA JAMAA WATATUUA

CHONDE CHONDE GAVANA WANGU WA BOT PROF LUOGA VAMIA PALE ATA LEO JIONI I SWEAR WAMEKAMATA KADI ZA BENKI ZA WANANCHI WANYONGE YANI MWANANCHI HANA ACCESS TENA NA MABO YA BENKI MPAKA WAKIMALIZA MAREJESHO YAO NDIO WANAKURUDISHIA KADI NA PASSWORD YAKO BAADA YA WAO KUTOA YA MWANACHI NA KUINGIZA ZA KWAO AISEEE NI HATAREEEEEEEEE.

MIAKA MITANO TENAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Nilishaliona pia hilo pale ATM za NMB Korogwe Kuna wakuria ofisi zao zipo jirani na Ofisi za Tigo Korogwe, nap ni hivyo hivyo .cha ajabu mtu ukikopa riba yao ni 50% huu wizi wa mchana

Hao wakopeshaji Ni wajanja sn... Utakuta Ana kiduka kidogo Cha vifaa Kama redio, tv nk... Sasa ule mkataba wa mkopo utasoma ulikopa kitu fulani na kitalipwa kwa mikupuo na riba kubwa..

Sio kwamba hawajulikani... Wanafahamika kwa kazi hiyo.

Tatizo Ni mikopaji kwenda kukopa kwa hiari yake... Pasipo kutoa taarifa sehemu husika Kama tra au bot...

Mbaya zaidi wanatumia risiti za Kuandika kwa mkono.
 
KUNA TAASISI MOJA YA KIFEDHA INAPATIKANA HAPA MWENGE KIVULINI.AISEEE HAWA JAMAA WANAWAUMIZA SANA WALIMU WA SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI.MZEE BABA HAWA JAMAA WANAKUPA MKOPO LAKINI SHARTI LAO NI KWAMBA UNAWAPA KADI YA BENKI,UNAWAPA NA PASS WORD ZAKO, WANAKUTOA ADI KWENYE SIMU BANKING YAN ALAFU WANAINGIA WAO KWA PASSWORD ZAO MPYA,I UNAWAPA CODE ZOTE NDIO WANAKUPA MKOPO YANI.

RAIS WANGU MAGUFULI WAFUATILIE HAWA JAMAA WANAITWA MHELE COMMERCIAL AGENCY (MCA) WAPO HAPA MWENGE KIVULINI YANI UKIJARIBU KUFANYA SURPRISE VISIT WALE JAMAA UTAKUTANA NA KADI ZA BENK ZA WATEJA KAMA MIA MBILI NA USHEEE WAMEZIKAMATIA OFISINI KWAO. WANAWAFANYA WALIMU KAMA WATUMWA WAO.WANA DRAW HELA YAO THEN WEWE UAENDA KUCHUA KILICHOSALIA AISEEE HII NCHI HAWA JAMAA WATATUUA

CHONDE CHONDE GAVANA WANGU WA BOT PROF LUOGA VAMIA PALE ATA LEO JIONI I SWEAR WAMEKAMATA KADI ZA BENKI ZA WANANCHI WANYONGE YANI MWANANCHI HANA ACCESS TENA NA MABO YA BENKI MPAKA WAKIMALIZA MAREJESHO YAO NDIO WANAKURUDISHIA KADI NA PASSWORD YAKO BAADA YA WAO KUTOA YA MWANACHI NA KUINGIZA ZA KWAO AISEEE NI HATAREEEEEEEEE.

MIAKA MITANO TENAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Haya ndio tunayoyasema alafu kuna watu wanatetea. Very bad!!
 
Back
Top Bottom