BoT fanyeni msako wa kushitukiza, bado ziko taasisi za kifedha zinazokaa na kadi za benki za wateja wao

Mimi nadhani sheria ingekuwa inawagusa wote,yaani mwenye kadi na mkopeshaji wote wawajibishwe. Maana haiwezekani mtu akope mwenyew bot waingilie et kwa kuwa kaacha kadi. Yaan mtu akikopa anaanza kuona uchungu kulipa ndio anaenda kuchongea.
 
Mimi nakopesha bila leseni kwa riba kubwa na ninafanya blogging bila leseni.

Haya kashtakini BoT na TCRA nikamatwe. Swine
Wamekusikia na watakufikia💣👍
 
Control za wateja wasio waaminifu, kuna hii ninayo fahamu mimi kama una mkopo na bank X basi ukitoa hela kwa kadi lets say punde mshahara unapoingia tambua huwa kuna penalt kwa kutofanya marejesho kwa huo mwezi, na penalti huwa ni kubwa sana unaweza shangaa siku unaomaliza mkopo wako wataendelea kukata hata kwa mieze miwili au mitatu zaidi ,imemtokea rafiki yangu hii, ndugu nimeshangaa unaposema kuna bank wanakaa na kadi za wateja, ni bank gani hizo mkuu, security za mkopo wako ni kazi/ajira yako uliyonayo na sio kadi za atm,
 
Soma vizuri uelewe.
 
Hawajakupora
Wengine wanakabidhi hadi bima za afya
Na sasa wanachukua mpaka vyeti, na vitambulisho kama dhamana
Hali tete
Kadi za bima jamani zinahusiana nini na mkopo wako, ukikubali basi nikutokuelewa unakua kama hujasoma mkataba wa mkopo wako maana kwenye mkataba kuna masharti ya kuomba mkopo na hivyo vingine mara nyingi havipo kwenye karatasi ya mkataba inakuje mnakubali kuchukuliwa kadi zenu za bima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…