BoT: Hatua za kisera kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa Sekta Binafsi na kupunguza viwango vya riba

Hongera benki kuu na serikali kuja na mkakati huu.

Hii ni hatua nzuri sana.

Haya ndiyo mambo ya kishua tunayotaka.
 
Sisi tunataka katiba mpya, sera sera hizi tumezisikia tangu Mwalimu ila umaskini ndiyo unatahamalaki.
 
Lakini pia riba ikiwa chini sana sekta ya benki inaweza kufa au kudorora.
 
Naipongeza BOT kwa sera hii ila kushusha ghafla had 10 bank hazitataka atleast tungeanzia 13 then tuwalete 10
 
Lakini pia riba ikiwa chini sana sekta ya benki inaweza kufa au kudorora.
Sidhan sana,Moja ya vitu vikubwa vilivyokuwa vinachangia riba za mabenki ya biashara kuwa kubwa ni pamoja na gharama za riba za mikopo wanayolipia kutoka benki kuu kuwa kubwa mno na kuna wakati walikuwa wanakopeshwa kwa rate ya zaid ya 10%
 
Tatizo kubwa ni dhamana ya kuchukua hiyo mikopo, pesa haitolewi kama karanga!

Mortgage....Vijana wanaambiwa wakajiajiri..hayo ni matamko ya wanasiasa, waliofilisika mawazo.

Kijana Hana dhamana, suluhisho ni Nini?

BOT inaongelea hawa wafanyabiasha wachache...chain ile ile?

Waziri wa fedha, na wachumi wote...BOT wameshindwa kuja na suluhisho la kutanua wigo wa walipa Kodi?

Vijana wanazo mbinu za biashara, ila wamenyimwa fursa Kwa sababu ya kuporwa Haki. Wabunge wanapewa mabillion ya mafao, ila Sekta binafsi NSSF kupewa FAO la KUJITOA. Ni ngumu.

Watu skilled, wakimaliza mkataba..hawapewi Haki zao. Serikali inachukua pesa, inapeleka kwenye White elephant projects.

Tulipe tu Tozo...au twende Burundi
 
Ndiyo wangefanya hivyo, yaani wangeweka kipengele kuwa ili Benki iwe na Sifa ya kupewa Mkopo wa 3% kutoka Benki Kuu Sharti hiyo Benki itoze Riba ya 10% kwa Wateja wake.

Kusema kweli hizi Riba za haya Mabenki zimekuwa kero sana kwa wateja, yaani mkopo wa 13,000,000 unarudisha 26,000,000. Ni nyingi Sana aisee
 
Nafuu hapo ni kwa mawakala tuu lakini hilo sharti (i) halitekelezeki,lilitakiwa kuwa sharti la jumla badala ya kulazimisha mabenki kukopesha kwenye sekta ya kilimo .

Sekta ya kilimo ni risk Sana kwa mantiki hiyo benki Zita kacha hilo sharti Ili waendelee na utaratibu wao wa siku zote,kuna benki ya kilimo hiyo ndio BOT wangeilenga specifically
 
Nimeona wameweka hivyo kwenye kipengele cha nne ( IV) cha hiyo barua iliyoambatanishwa hapo juu.
 
Sharti la ujumla nadhan limezungumzwa kwenye kipengele namba nne kama sijakosea (IV).
 
Nimeona wameweka hivyo kwenye kipengele cha nne ( IV) cha hiyo barua iliyoambatanishwa hapo juu.
Waisisitize, ikiwezekana waweke na faini kabisa. Hizi benki hazina huruma kabisa
 
Hii imekaa vizuri!!!
 
Sharti la ujumla nadhan limezungumzwa kwenye kipengele namba nne kama sijakosea (IV).
Hii imekaa ki optional zaidi but nilitegemea BoT iruhusu mabenki kutafuta mitaji kokote kwenye masoko ya mitaji ndani na nje ya nchi badala ya kutegemea ndani tuu na kwao Ili kuongeza ukwasi zaidi,wao BoT wawe approval Ili kudhibiti kiwango cha pesa nk
 
Benki kuu ni regulator na ndiye anayeset riba ya base point. Nadhani enki zinacharge kufuatana na riba inayotolewa na benki kuu. Kama riba inayowakopesha ni ndogo lazima benki zitashusha riba. Ila benki nyingi hawana mitaji ya kutosha wakati demand ya mikopo ni kubwa sana, ndiyo maana riba ni kubwa.

Pia riba inayotozwa kwenye amana ni kubwa hivyo benki nyingi hazikopeshi bali hununua amana za serikali na hii inazidi kupunza fedha ambazo zingetolewa kama mikopo kwa watu binafsi. hence riba kuwa kubwa kwa mikopo.

Solution ni riba za bonds ba treasury bills zishushwe ili mabenki yapendelee kukopesha kwa watu binafsi badala ya kufanya biashara na serikali. Hii ni ngumu kutekelezeka maana serikali ina uhitaji mkubwa wa fedha hivyo lazima itakopa tu, so sijui itakuwaje. Tusubiri tuone.
 
Waisisitize, ikiwezekana waweke na faini kabisa. Hizi benki hazina huruma kabisa
Nakuhakikishia lazima riba zitashuka-Ukiangalia hzo sera kiujumla kwa mapana utagundua wamekwisha ingilia directly or indirectly,Example-Makampuni ya simu (VODACOM,AIRTEL,TIGO etc,) huwa yana ukwasi mkubwa sana wa kifedha ambazo huzitumia kwenye biashara kwa kuzikopesha benki za biashara kwa riba shindani-sasa hapo kwenye sera wamepewa limit ya riba ambayo wanapaswa ku-charge wanapokopesha taasis nyingine za kifedha hvyo itasaidia kushusha riba kwenye soko.
 
Mbona walengwa hapo ni wakulima?kwa sisi wamachinga haituhusu tuendelee na vikoba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…